Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, May 7, 2013

WATU WATATU WAMEFARIKI DUNIA KATIKA MATUKIO TOFAUTI MKOANI NJOMBE LIKIWEMO LA KUJINYONGA.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani akiwa ofisini kwake na waandishi wa habari jana.

Watu Watatu Wamefariki Dunia Katika Matukio Tofauti Mkoani Njombe Likiwemo la Mkazi Mmoja wa Kijiji Cha Idihani Kata ya Lugenge,Aliefariki Baada ya Kuungua Moto Akiwa Nyumbani Kwao.

Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe ACP Fulgency Ngonyani Amemtaja Mtu Huyo Kuwa ni Esta Mwalongo Aliefariki Baada ya Kuungua Moto Wakati Akiwa Jikoni Nyumbani kwake na Kusema Kuwa Taarifa za Awali Zinaonesha Kuwa Marehemu Alikuwa na Ugonjwa wa Kifafa.

Amesema Tukio Hilo Limetokea May Tatu Mwaka Huu na Kuongeza kuwa Jeshi la Polisi Linaendelea na Uchunguzi wa Tukio Hilo.

Katika Tukio lingine Mkazi Mmoja wa Ubena Makambako Amefariki Dunia Baada ya Kujinyonga Kwa Kutumia Kamba aina ya Manira Wakati Akiwa Nyumbani Kwake.

Kamanda Ngonyani Amemtaja Mtu Huyo Kuwa ni
Ella Mkonde Ambae Alikutwa Amejinyonga chumbani kwake mnamo mei 3 mwaka huu na Hivyo Jeshi la Polisi Linaendelea na Uchunguzi Juu ya Tukio Hilo.

Wakati Huo Huo Mkazi Mmoja wa Mjimwema Makambako Amefariki Dunia Baada ya Kugongwa na Gari Katika Barabara ya Njombe-Makambako Katika Kijiji Cha Ngamanga Wakati Akiendesha Baiskeli.

Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi Fulgency Ngonyani Amesema Tukio Hilo Limetokea May Tano Mwaka Huu na Kumtaja Mtu Huyo Aliefariki Kuwa ni Aloyce Kaduma Ambae Aligongwa na Gari Yenye Namba za Usajili T 737 CJU Aina Ya Toyota Hiace Mali ya Joseph Mwangiri Mkazi wa Songea Mkoani Ruvuma.

Akifafanua Chanzo Cha Ajali Hiyo Kamanda Ngonyani Amesema ni Kutokana na Kupasuka Kwa Tairi ya Gari na Hivyo Kusababisha Gari Hilo Kuyumba na Hatimae Kumgonga Marehemu Aliekuwa Akiendesha Baiskeli pembeni mwa barabara hiyo.

Amesema Jeshi la Polisi Linaendelea na Uchunguzi wa Tukio Hilo na Hivyo kutoa Wito Kwa Wananchi Kushirikiana na Jeshi la Polisi Ili Kuweza Kuwabaini Wahusika na Kuwataka Madereva Kuwa Makini Pindi Wanapokuwa Barabarani Ili Kuhepuka Matukio Kama Hayo.

Kumekuwa na Matukio ya Mara Kwa Mara ya Ajali za Barabarani Mkoani Njombe Ambayo Pamoja na Madhara Mengine Pia Yamekuwa Yakisababisha Vifo Kwa Wananchi hapa nchini.

No comments:

Post a Comment