WANAUMISETA WA KUTOKA WILAYA MBALIMBALI MKOA WA NJOMBE WAKIFANYA GWARIDE MBELE YA MGENI RASMI
WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI KUTOKA WILAYA ZA MKOA WA NJOMBE WAKIWA WAMEONGOZANA NA MAAFISA MICHEZO WA WILAYA NA MIJI.
KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMBE MGEN BARUANI AKITOA HOTUBA KWA WANAUMISETA LEO KATIKA UWANJA WA SHULE YA SEKONDARI NJOMBE.
WALIMU KUTOKA SHULE MBALIMBALI ZA HALMASHAURI ZA MKOA WA NJOMBE WAKIMSIKILIZA KWA UMAKINI MGENI RASMI KATIKA HOTUBA YAKE.
AFISA MICHEZO WA MKOA WA NJOMBE STIVIN SANGA AKIENDESHA RATIBA YA MICHEZO YA UMISETA MBELE YA MGENI RASMI WAKATI WA UFUNGUZI HUO.
KATIKATI NI KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMBE MGENI BARUAN AKIWA NA AFISA ELIMU MKOA WA NJOMBE AMBAE NI MWENYEKITI WA MASHINDANO YA UMISETA MKOA SAID NYASIRO ALIYEVAA KOTI JEUSI PAMOJA NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE PAULO MALALA TRACK SUTI YA RANGI YA NJANO.
MGENI RASMI KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMBE MGEN BARUAN AKIKAGUA TIMU YA MPIRA WA MIGUU KWA WASICHANA AMBAO WAMEANZA BAADA YA UFUNGUZI WA MASHINDANO HAYO.
UWANJANI HUMO NI PAMBANO LA MPIRA WA MIGUU KATI YA TIMU YA WASICHANA WA KUTOKA HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO NA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE.Na Michael Ngilangwa,Njombe.
Akizungumza wakati wa kufungua mashindano ya michezo ya UMISETA katika ngazi ya mkoa katibu tawala wa mkoa wa Njombe bi.Mgen Baruani amewataka wanafunzi waliochaguliwa kuongeza bidii ili waweze kuchaguliwa kwaajili ya mashindano ya kanda na mkoa wa Njombe kwa pamoja ili kuongeza idadi kubwa ya washiriki wa mashindano watakaochaguliwa kuunda timu ya kanda na kufanya vizuri kitaifa.
Amesema mashindano hayo yanaumuhimu mkubwa kwa wanafunzi ikiwemo kusaidia kujenga udugu miongoni mwa wanafunzi walimu na washiriki wengine,kujifunza mazingira ya kijiografia,kugundua vipaji mbalimbali ambavyo ni hazina kubwa ya wanamichezo katika taifa la Tanzania,kujenga afya ya wanafunzi,kukuza utamaduni wa mtanzania,kujenga umoja miongoni mwa wanafunzi na kupata taifa lenye amani na ustawi bora pamoja na kusaidia kuepukana na vishawishi vya utumiaji wa madawa ya kulevya,ulevi wa pombe na kujihusisha na masuala ya mapenzi katika umri mdogo ambapo matokeo yake ni kupatwa na maambukizi ya UMKIMWI.
Aidha BI Baruani amewaasa washiriki wote wa mashindano hayo kuchukua tahadhari kubwa kwa kipindi chote watakachokuwepo mkoa wa Njombe kujihadhari na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwani mkoa wa Njombe unaongoza huku akiipongeza halmashauri ya wilaya ya Njombe kwa kukamilisha michango ya fedha katika michezo hiyo na kuzitaka halmashauri nyingine ambazo hazijakamilisha michango hiyo kukamilisha mara moja kwaajili ya mashindano hayo.
Amesema kutokana na kutambua umuhimu wa michezo kwa vijana ofisi ya mkuu wa mkoa wa Njombe inatarajia kutoa vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo viatu,track suti,soksi,mipira ya miguu,mikono na mipira ya meza kwa wanaumiseta hao.
Awali akitoa taarifa fupi ya mashindano ya UMISETA Afisa elimu wa shule za sekondari mkoa wa Njombe ambae ni mwenyekiti wa mashindano hayo bwana Said Nyasiro amesema kuwa mashindano hayo yalitegemewa kuwa na idadi ya wanamichezo 625 pamoja na viongozi 75 ambapo mpaka sasa wanawanamichezo 519 na walimu wa michezo 63.
Bwana Nyasiro amebainisha idadi ya wanamichezo waliopelekwa kwenye mashindano hayo na halmashauri za mkoa wa Njombe kuwa ni pamoja na Halmashauri ya mji wa Njombe imepeleka wanamichezo 125 ambapo kiwango hicho kinastahili kupelekwa kwenye mashindano hayo kwa halmashauri zote na waamuzi 12,halmashauri ya wilaya ya Njombe imepeleka wanamichezo 125 na viongozi 12,Ludewa wanamichezo 101 waamuzi 12,makete 44 na waamuzi 8,Makambako wamepeleka wanamichezo 124 waamuzi 10 ambapo ni chini ya idadi iliokusudiwa.
Aidha amesema mashindano hayo kwa mko yamejumulisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu kwa wavulana na wasichana,netbally kwa wasichana pekee,riadha,mitupo,kuruka mpira wawavu kwa wavulana na wasichana ambapo mashindano hayo ya mkoa yanadumu kwa muda wa siku tatu na baada ya hapo wataunda timu ya mkoa wa Njombe itakayokuwa na wanamichezo 125 na viongozi 12 ambayo itabaki kambini kuanzia mei 28 mpaka june mosi huku watakaoshindwa mkuingia kwenye timu ya mkoa watarudishwa kwenye vituo vya.
Amesema kuwa baada ya hapo timu hiyo ya mkoa itakwenda mkoani Ruvuma wilaya ya Songea ambako kutakuwa na mashindano ya UMISETA kwa mikoa mitatu Iringa Njombe na Ruvuma ambapo baada ya kupambanishwa kimikoa na mashindano huko Songea yataanza june 3 na ifikapo june 5 wataunda timu ya kanda na june 9 wataanza safari yakuelekea Kibaha ambako kitaifa yatafanykia huko baadae timu hizo zitarudishwa katika vituo vyake .
Amesema uhaba wa fedha ni miongoni mwa changamoto kubwa ikiwemo uhaba wa fedha ambapo katika mmashindano hayo walitarajia kupata fedha hizo kutoka katika halmashauri na karo za wanafunzi na kwamba katika karo za wanafunzi walitarajia kupata takribani milioni 39 ambapo mpaka sasa ni halmashauri ya wilaya ya Njombe pekee ndiyo iliyokwisha kuchangia,vifaa vya michezo ni miongoni mwa changamoto,viwanja vya michezo,muamko mdogo kwa wadau kuchangia michezo huku akizitaka halmashauri kuwasilisha michango hiyo mapema ili mashindano hayo yaendelee.
No comments:
Post a Comment