Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, May 24, 2013

MADEREVA BODABODA LEO WAANZA KUTENGENEZA BARABARA KWA KUFUKIA MADIMBWI BARABARA YA STENDI HADI KIHESA.












Hizi ni bodaboda zao wamezipaki wakati wakitengeneza barabara hiyo kwa kufukia makorongo leo.
Hii ni barabara ya kuanzia kituo cha mabasi cha Njombe kueekea mtaa wa kihesa wanayoweka kifusi ili kusafiri na bodaboda kwa urahisi.
Makamu mwenyekiti wa waendesha pikipiki mkoa wa Njombe maarufu kwa jina la bodaboda Emiram Msigwa akihojiwa na mwaandishi wa habari.

Mzee msigwa nae amewaunga mkono madereva wa bodaboda katika kutengeneza barabara hizo na hapa anahojiwa na waandishi wa habari.
Abell Mgaya ni mwenyekiti mstaafu nae alikuwepo kwenye tukio hilo na akaunga mkono jitihada hizo. Picha na Michael Ngiangwa.


Katika Kile Kinachoonekana Kuwa ni Kuchoshwa na Ubovu wa Barabara Zinazounganisha Maeneo Mbalimbali ya Mji wa Njombe,Madereva wa Bodaboda Wa Kituo Kikuu Cha Mabasi Mjini Njombe Wameamua Kuunganisha Nguvu Zao na Kujaza Kifusi na Kuziba Mashimo ya Barabara ya Mtaa wa NHC Kuelekea Kihesa na Kupunguza Kero Kubwa Iliokuwa Ikiwakabili.

Wakizungumza na Uplands Fm,Wamiliki na Madereva wa Bodabod Wamesema Mara Kadhaa Kumekuwa Kukijitokeza Matukio ya Ajali Kwenye Barabara Hiyo Ambayo Kwa Sehemu Kubwa Yamekuwa Yakisababishwa na Ubovu wa Barabara.

Emiramu Msigwa ni Mhasibu wa Umoja wa Madereva wa Bajaji Mjini Njombe Anasema Uamuzi wa Kuweka Kifusi Kwenye Barabara Hiyo,Unatokana na Kuongezeka Kwa Wateja wa Maeneo Hayo na Hivyo Kuiomba Serikali Kuwasaidia Katika Kuboresha Miundombinu Iliopo Kwasasa.

Nao Baadhi ya Madereva wa Bajaji Wamewaomba Madereva Wengine Kujitokeza kushiriki Zoezi Hilo,Lililolenga Kuboresha Sekta ya Usafiri wa Umma na Kuifanya Yenye Uhakika Zaidi Mkoani Njombe.

Wamesema zoezi hilo litakuwa ni endelevu kwa kujaza kifufu cha udogo katika maeneo yote ambayo hayapitiki kwa pikipiki na kuhepusha ajali zisizo za lazima.

No comments:

Post a Comment