Thursday, May 9, 2013
JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE LA FANIKIWA KUKAMATA MAJAMBAZI WAWILI MMOJA ALIKAMATWA BAADA YA KUPIGWA RISASI NA POLISI ALIPOKUWA AKIJARIBU KUKIMBIA..
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Fulgence Ngonyani akiongea na waandishi wa habari ofisini kwakejana.picha na Michael Ngilangwa.
Naibu Mkuu wa upelelezi mkoa wa Njombe Florence Ibrahimu Mwenda akiwaonesha waandishi wa habari risasi zilizopigwa na polisi hatimae kupasua tairi ya gari na baadae kumpiga risasi jambazi mmoja mpka kukamatwa eneo la mahakama ya wilaya ya Njombe wakikimbia kuelekea barabara ya makambako.picha na Elia Kayombo
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linawashikilia Watu Wawili Kwa Tuhuma za Kuhusika na Jaribio la Wizi Katika Kijiji Cha Nundu Wilayani Njombe.
Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi Fulgency Ngonyani Amewataja Watu Hao Kuwa ni Wasia Abduli 28 Ambae Alikamatwa Baada ya Kupigwa Risasi Mguuni Pamoja na Yasini Mstaafa 29 Wote Wakazi wa Songea Mkoani Ruvuma.
Amesema Mnamo May 6 Mwaka Huu Majira ya Saa Nne Usiku,Askari Polisi Waliokuwa Doria Walipata Taarifa za Kuwepo Kwa Jaribio la Wizi Katika Kijiji Cha Nundu na Hivyo Kufika Kwa Ajili ya Kuimarisha Ulinzi na Usalama wa Eneo Hilo.
Ameongeza Kuwa Baada ya Askari Hao Kufika Eneo Hilo Walifanikiwa Kuliona Gari Aina ya Toyota Chesa Yenye Namba za Usajili T T908 AAR Ikiwa na Watu Watatu Ambao Licha ya Kuwataka Kujisalimisha Hawakuweza Kufanya Hivyo.
Imedaiwa kuwa majambazi hao walikodi gari hilo kwa mtu mmoja wa Songea mkoani Ruvuma ambae hakufahamika jina lake kwa shilingi laki nne na alipo sema awapeleke walikataa na kusema kuwa wanaelekea mkoani Mbeya.
Katika Tukio Jingine Jeshi Hilo Linamshikilia Mkazi Mmoja wa Tunduma Mkoani Mbeya Betelis Mwampashe Kwa Tuhuma za Kukutwa na Vipodozi Vilivyopigwa Marufuku na Serikali.
Wakati Huo Mkazi Mmoja wa Mji Mwema Mjini Njombe Amefariki Dunia Baada ya Kunyongwa na Kisha Kupigwa na Kitu Kizito na Kufariki Dunia Katika Kijiji Cha Magoda Wilayani Njombe.
Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe Fulgency Ngonyani Amesema Tukio Hilo Limetokea Jana na Kusema Kuwa Jeshi Hilo Bado Linaendelea na Uchunguzi wa Tukio Hilo Ili Kuweza Kubaini Waliohusika na Kitendo Hicho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment