Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, May 12, 2013

ALIYEKUWA KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WILAYA YA NJOMBE ERNEST MACHUNDA AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMUKIA LEO JUMAPILI..

Aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Njombe  bwana Ernest Machunda enzi za Uhai wake.
Aliekuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Njombe Ernest Machunda Amefariki Dunia Wakati Akipatiwa Matibabu Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoani Mbeya.
Taarifa Iliotolewa na Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe Imesema Marehemu Alifariki May 11 Mwaka Huu Mara Baada ya Kufikishwa Hospitalini Hapo Kwa Matibabu.
Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Hosea Mpagike Amesema Chama Hicho Kimepokea Kwa Masikitiko Makubwa Taarifa Hizo Hasa Ikizingatiwa Kuwa Marehemu Katika Uhai Wake Akiwa Mtumishi wa CCM Alioonesha Uhodari Mkubwa wa Kazi.

Nacho Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Njombe Kupitia Kwa Kaimu Katibu Wake Alatanga Nyagawa Kimetuma Salamu za Rambirambi Kwa Uongozi wa CCM Mkoa wa Njombe Kufuatia Kifo Hicho.

Marehemu Ernest Machunda Alianza Kazi Mkoani Njombe Akiwa ni Katibu wa CCM Wilayani Njombe Kwa Zaidi ya Mwaka Mmoja Sasa Baada ya Njombe Kupandishwa Hadhi na Kuwa Mkoa  Rasmi Akichukua Nafasi ya Hosea Mpagike Ambae Alipanda na Kuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe.



Maandalizi na taratibu za mazishi yanafanykia nyumbani kwake alikomjenga mkoani Mbeya.
Mwili wa marehemu unatarajia kusafirishwa kesho 13 mei mwaka huu kwenda Musoma -Butiyama kwaajili ya mazishi na kwamba Mkoa wa Mbeya alikuwa na makazi ikiwa alijenga wakati akiwa kazini kabla ya kuhamia mkoa wa Njombe. 
MUNGU Ailaze Roho ya marehemu ERNEST  MACHUNDA Mahali pema peponi AMEN.

No comments:

Post a Comment