Mbowe Ampa Pole Katibu wa Baraza la Vijana Chadema kwa Kufiwa na Baba yake Mzazi
MWENYEKITI
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe leo
Jumapili alikwenda kumpa pole Katibu wa Baraza la Vijana wa CHADEMA
(BAVICHA), Deogratias Munishi kutokana na msiba baba yake mzazi, Mzee
Ephraimu Sabinus Munishi. Kiongozi huyo alifika kuijulia hali familia ya
marehemu eneo la Sinza Uzuri, Dar es Salaam, jana. Mazishi ya marehemu
Munishi yanatarajiwa kufanyika Kilimashuku, Maili Sita, Moshi, Jumaane
wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment