Lwakatare aligawa Bunge
LISSU APANGUA TUHUMA ZA MWIGULU KWA CHADEMA
SAKATA la
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Wilfred Lwakatare na Ludovick Rwezaula kushtakiwa kwa makosa
ya ugaidi, limeibua mvutano mkali bungeni huku wabunge wakishambuliana
kwa maneno makali.
Mvutano huo
uliibuka jana wakati wa kujadili hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri
Mkuu kwa mwaka wa fedha 2013/2014 ambapo Mbunge wa Iramba Magharibi,
Mwigulu Nchemba (CCM) alichafua hewa wakati akichangia na kudai kuwa
aliyerekodi video ya Lwakatare yupo tayari kuja kutoa ushahidi.
Mwigulu
ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) aliliambia Bunge kuwa
CHADEMA wasihangaike kujitetea kwa swala la Lwakatare kwani ushahidi
wote kuhusu video hiyo upo na kwamba yuko tayari kuutoa bungeni, duniani
na mbinguni.
“Nataka
nitoe ufafanuzi kuhusu suala la ugaidi ambalo Mwenyekiti wa CHADEMA,
Freeman Mbowe amezungumza kwenye hotuba yake hapa bungeni jana.
Aliyerekodi mkanda yupo na mimi niko tayari kuhojiwa popote hata
mbinguni,” alisema Mwigulu na kuibua nderemo kutoka kwa wabunge wa CCM.
Mwigulu
alionyesha karatasi aliyodai kuwa ilitumiwa na Lwakatare kupanga kile
alichodai kuwa ni mkakati wa mauaji akisema huo ndiyo mkakati wa CHADEMA
kupanga mauaji na kwamba viongozi wakuu wa chama hicho wanapaswa
kushtakiwa.
Bila kujali
kwamba suala hilo liko mahakamani wala ni kinyume cha kanuni za Bunge
kumtaja mbunge mwingine kwa jina akimtuhumu, Mwigulu alisema anaishangaa
CHADEMA kumtaka yeye aunganishwe kwenye kesi kwa kuwa na mawasiliano na
mmoja wa watuhumiwa wakati hata wao wana mawasiliano na Lwakatare.
“Alisema
Mbowe hapa jana kuwa mimi napaswa kushtakiwa kwa ugaidi, ingawa simuoni
hapa ndani labda tayari amekwishakamatwa na polisi, lakini nataka kusema
kuwa watu hawa ni waongo na wanafiki. Wanapanga mauaji halafu wanakuja
hapa kuwahadaa wananchi kuwa wanapinga ugaidi,” alidai.
No comments:
Post a Comment