Kesi ya Mauwaji ya Mtoto Dorisi Lutego Inayowakabili Watuhumiwa Watano Akiwemo Mganga wa Jadi Sharif Jabiel Ngairo Sagasaga Imetajwa Tena Leo Katika Mahakama ya Wilaya ya Njombe.
Akisoma Hati ya Mashtaka Mbele ya Hakimu wa Mahakama Hiyo Agostino Lwezile ,Mwendesha Mashtaka wa Polisi Serapian Matiku
Ameiambia Mahakama Kuwa Faili la Kesi Hiyo Bado Lipo Kwa Mwanasheria Mkoani Iringa na Hivyo Kesi Hiyo Kushindwa Kupangiwa Tarehe ya Kutajwa Tena.
Watuhumiwa Wengine Wanaotuhumiwa Kuhusika Katika Mauwaji Hayo ni Robert George Mgeni,Christopha George Mgeni,Michael Mkarius Msemwa na Egno Mgaya Wote Wakazi wa Wilaya ya Njombe.
Watuhumiwa Hao Wanadaiwa Kutenda Kosa Hilo Juni 12 Mwaka 2011 Katika Shule ya Livingstone Mjini Njombe , Ambapo Watuhumiwa Hao Walivamia Bweni Alilokuwa Akiishi Mtoto Huyo.
Wakati Huo Huo Mahakama Hiyo Imewaachia Huru Watuhumiwa Wanne Akiwemo Enerico Kiwale Aliyeachiwa Huru Baada ya Ushahidi Uliotolewa na Upande wa Mashtaka Kutojitosheleza Pamoja na Kutowasilisha Vielelezo Vilivyotajwa.
Mahakama Hiyo Pia Imewaachia Huru Oscar Richard Ruvalamo , Jairos Maarufu Kwa Jina la Lupipa na Bosco Ngole Waliokuwa Wakikabiliwa na Makosa ya Mauwaji ya Sylvesta Mgina Mkazi wa Kijiji cha Kifumbe Wilayani Njombe.
Akisoma Hukumu ya Kuachiwa Kwa Watuhumiwa Hao , Hakimu John Kapokolo Amesema Watuhumiwa Hao Wameachiwa Baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali Kutokuwa na Haja ya Kuendelea na Kesi Hiyo na Kwamba Shtaka Hilo Limeondolewa Chini ya Kifungu cha 91 Kifunngu Kidogo cha Kwanza cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai Kama Ilivyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2002
No comments:
Post a Comment