Tuesday, March 19, 2013
ZAIDI YA WAKAZI 1000 MBIONI KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI KATIKA KIJIJI CHA LIMAGE NJOMBE.
Mgeni rasmi akirejea mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji katika kijiji cha Limage wakati wa wiki ya maji halmashauri ya Mji wa Njombe.
Uzinduzi wa mradi wa maji Limage wenye thamani zaidi ya shilingi milioni mia Mbili ukiwekwa jiwe la Msingi leo na Diwani wa kata ya Yakobi Bi.Esther Mgeni.
Hapa msafara ukiwa umetoka kusaini kitabu cha wageni katika ofisi ya kijiji cha Limage ukielekea kukagua mabomba na kisha kuweka jiwe la msingi katika mRADI huo.
Mgeni rasmi Esther Mgeni akizindua mradi wa maji kwa kuweka jiwe la msingi kijijini Limage leo.
Mzee akishukuru hatua iliyofikiwa katika mradi wa maji kijijini humo leo.
Wazee nao hawakuwa nyuma kushangilia mradi huo,wasema adha ya maji itapungua kijijini humo.
Diwani wa kata ya Yakobi Akisindikizwa kwa shangwe mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa maji kijijini Limage leo.
Haya ni mabomba ya mradi huo wa maji uliowekwa jiwe la Msingi leo na diwani wa kata ya Yakobi.
Malalamiko ya wananchi wa kijiji cha Limage kata ya Yakobi juu ya kusuasua kwa mradi wa maji waliochangia michango yao umeanza kutekelezwa rasmi hivi sasa.
Hatua hiyo imekuja kufuatia kuwekwa kwa jiwe la msingi la mradi huo wenye thamani zaidi ya shilingi milioni 200 utakaohudumia watu zaidi ya mia moja katika muendelezo wa matukio ya wiki ya maji iliyozinduliwa machi 16 mwaka huu kitaifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment