Baadhi ya Wakristo wakatoliki wakiwa na matawi ya mizeituni kufunya kumbukumbu ya kumpokea mwokozi wao kama walivyofanya wana wa Yerusalemu. |
Waamini wakiwa na matawi mbele ya jukwa la Kichangani wakisubiri Padre ayabariki ili kuanza maandamano kuelekea kanisani. |
Waamini wakiwa kwenye maandamamo yaliyoanzia Kichangani kuelekea Kanisa Kuu la Kiaskofu Kihesa. |
Wanakwaya wa Kwaya ya Mt. Cecilia Parokia ya Kihesa wakiwa kwenye maandamamo kuingia Kanisani. |
Na Gustav Chahe,
Iringa
USALITI wa kisiasa umetajwa kuwa
ni chanzo cha unyonyaji na dhuruma ya haki za wengine.
Haya yamezungumzwa na Padre
Ponsiano Myinga wakati wa maadhimisho ya Misa Takatifu iliyofanyika leo katika
Kanisa Kuu la Kiaskofu Parokia ya Kihesa.
Amesema usaliti umezaa
udanganyifu na upotoshaji wa mambo ya wazi na kusababisha mitafaruku ya isiyo
ya lazima.
Amesema usaliti unatokana na watu
kutumia rushwa katika kuhadaa haki za wananchi wasio na sauti.
Amemtaka kila mmoja kutimiza
wajibu katika nafasi yake kwa kutenda haki na usawa ili mwingine asiumie au
kuumizwa kwa ajili yake.
Aidha amesema kutokutimiza wajibu
kwa uaminifu ni kumsaliti Kristo.
Wakristo nchini wanaungana na
wakristo wote duniani kufanya kumbukumbu ya kumpokea Yesu Kristo akitokea
Caprenaum kwenda Yerusalem wakiwa na matawi ya mizeituni wakimshangilia na
kumlaki.
No comments:
Post a Comment