Wananchi
wa kijiji cha kifanya wakiwa kwenye mkutano wa hadhara jana wakati
wakiazimia kuuza miti ya kijiji kwa ajili ya ujenzi wa maendeleo
mbalimbali.
Huyu ni afisa mtendaji wa kijiji cha
Kifanya bwana Blasius Mchami akieleza baadhi ya mashine zinatarajiwa
kuanza kazi baada ya kukamilika kwa jengo lake.
Wananchi wa
Kijiji cha Kifanya na Uongozi wa Kijiji Hicho Kwa Pamoja Wamekubaliana
Kuuzwa Kwa Miti ya Msitu wa Kijiji Hicho Ili Kupata Kiasi cha Shilingi
Milioni 60 Kwa Ajili ya Kukamilisha Miradi Mbalimbali ya Maendeleo
Kijijini Humo.Makubaliano Hayo Yamefikiwa Jana Kwenye Mkutano wa Hadhara wa Kijiji Hicho na Kuongeza Kuwa Fedha Hizo Zitatumika Kukamilisha Ujenzi wa Mradi wa Mashine ya Kusaga Unga ya Kijiji Hicho, Ukarabati wa Madarasa , Ujenzi wa Nyumba Mbili za Walimu, Pamoja Ununuzi wa Madawati.
Wakizungumza Kwenye Mkutano Huo Afisa Mtendaji na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kifanya Bwana Blasius Mchami na Bwana Bosco Mtewele Wamesema Miti Hiyo Inatarajiwa Kuuzwa Kwa Shilingi Milioni 58 na Kwamba Miti Hiyo Itauzwa Kwa Njia ya Mnada Ili Kumpata Mnunuzi Atakaye Nunua Kwa Bei ya Juu .
Aidha Viongozi Hao Wameongeza Kuwa Pamoja na Kukubaliana Kuuzwa Kwa Miti Hiyo Lakini Bado Kiasi cha Fedha Zinatakiwa Hazitoshi Kukamilisha Miradi ya Maendeleo ya Kijiji Hicho na Hivyo Kutahitajika Uongozi wa Kijiji na Wananchi Kukaa Pamoja na Kujadili Jinsi ya Kufikia Kiasi cha Shilingi Milioni Sitini Zinazohitajika.
Pamoja na mambo mengine wananchi wa kijiji hicho wameitaka serikali ya kijiji kwenda kufuatilia taarifa ya ukaguzi wa mahesabu mbalimbali iliyopelekwa Halmashauri ya mji wa Njombe ili kuendana na kasi ya kimaendeleo.
Mkutano Huo Umefanyika Jana Baada ya Kushindwa Kufanyika Wiki Iliyopita Kutokana na Idadi Ndogo ya Wananchi Waliohudhuri Kwenye Mkutano Huo.
No comments:
Post a Comment