Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, February 23, 2013

TAMKO LA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA MBEYA KUHUSU UCHOCHEZI WA KIDINI

MWENYEKITI
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA-MBEYA
NORMAN SIGALLA 
BAADHI YA VIONGOZI WA
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA-MBEYA
MWANDISHI WA HABARI FELIX MWAKYEMBE AKIULIZA SWALI KWA KAMATI HIYO
EMMANUEL LENGWA  MWANDISHI  AKIULIZA SWALI KWA KAMATI HIYO YA ULINZI YA MKOA WA MBEYA
MOJA YA WANAKAMATI YA ULINZI MKOA WA MBEYA KAMADA DIWANI AKIJIBU BAADHI YA MASWALI YALIOULIZWA NA WAANDISHI WA HABARI 


TAMKO LA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA MBEYA KUHUSU UCHOCHEZI  WA KIDINI
Kwanza kabisa tungependa kutoa pongezi kwa Viongozi na Waumini wa Dini na Madhehebu mbalimbali hapo Mkoa Mbeya kuendeleza utamaduni wetu wa kuishi na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii. Bila kuweka hisia za udini. Tunawashukuru kwa kuendelea kuvumiliana. Pamoja na kuendelea katika hali hii, kumejitokeza viashiria mbalimbali vyenye kuonyesha dalili za kumomonyoka kwa maadili, katika Mkoa wetu.
    2.   Kumejitokeza baadhi ya viongozi wa dini ambao wamekuwa   
Wakuzitumia nyumba zetu takatifu za Ibada kuhubiri mambo  ambayohayahusiani kabisa na mambo yanayohusu Mwenyezi Mungu na mafundisho yake, kwa kuhubiri mambo ya siasa za chuki kwa dhamira ya kupandikiza chukidhidi ya Serikali au dini na madhehebumengine. Baadhi yao wamediriki kuyasema hayo hadharani kwenye miadhara yao au mikusanyiko ya waumini wao.
   Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya inaona hali hii haina  
   afya njema kwa mustakabali wa amani na utulivu wa Mkoa wetu na    
   Nchi kwa ujumla.
3.               Pamoja na mahubiri hayo pia kumekuwepo nyaraka mbalimbali za kimaandishi za sauti katika kanda, CD zenye kuhubiri chuki, uchochezi dhidi ya dini au dhehebu lingine. Kumekuwepo na video katika kanda, CD au DVD zenye kuhubiri chuki, uchochezi, dharau na kebehi dhidi ya dini nyingine au Serikali na baadhi ya kanda hizo zimediriki kuhamasisha waumini wake vurugu na hata kuua jambo ambalo Kamti ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya inaamini hakuna dini ya aina yoyote dunianiinayohimiza waumini wote kutumia kwa jambo lolote lile.
4.               Baada ya kutafakari, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa  Mbeya imeamua yafuatayo:- inapiga marufuku:
(i)               Kuuza, kusambaza au kuonyesha, Kanda za sauti CD za sauti, Kanda   
za Video, CD, DVD, nyaraka na maandiko yoyte yenye uchochezi wa aina yoyote ile au kukashifu dini yeyote katika Mkoa wa Mbeya.
(ii)             Chombo chochote cha Habari kilichopo Mkoani Mbeya kiepuke   
           kuandika makala, kunakili au kurusha hewani hotuba, mahubiri au   
           kuonyesha video zenye kuchochea, kudharau, kuhubiri au kukashifu 
           dini yoyote ile 
  
5.       Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa inawaasa viongozi wa dini
 Mbalimbali kutohubiri siasa kwenye majumba ya Ibada kwani kwa   
 kufanya hivyo watakuwa wanakiuka sheria za nchi. Mtawagawa       
 waumini wenu kwa sababu waumini wanaelewa hayo si maagizo ya 
 Mungu, na hayamo kwenye vitabu vitakatifu.
6.       Waandishi wa Habari epukeni kushabikia matamko ya Viongozi wa   
          Dini au Siasa yenye kulenga kuleta mgawanyiko katika taifa hili kwa  
          Misingi ya kidini au kisiasa kwa kisingizio cha Uhuru wa Habari,  
          kumbukeni Amani Umoja na Mshikamano wa Mkoa na Taifa
          utategemea mchango wenu katika kushabikia au kukemea kauli hizo
          bila kujali zimetolewa na kiongozi gain.
Mwisho, Serikali itamchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayekwenda kinyume na haya, bila kujali itikadi yake, dini yake au wadhifa wake. Wananchi wanaaswa kuzikabidhi nyaraka, kanda CD na DVD kwa ofisi za Serikali ngazi ya Vijiji, kata Wilaya na Mkoa au kituo chochote cha Polisi. Endapo watakabidhi kwa hiyari hawatachukuliwa hatua.
Imetolewa na:
MWENYEKITI
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA-MBEYA

No comments:

Post a Comment