Hapa uongozi wa kata ya Ikuna akiwemo diwani wa kata hiyo bwana Valentino Hongori na afisa mtendaji wa kata hiyo Jobu Fute wakiwa kwenye kanisa lililoezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa.
Viongozi hao wa kata wanaelekea kwenye ofisi za kanisa la kkkt Matiganjora kuangalia jinsi lilivyoezuliwa na kuongea na wananchi.
Wananchi wamekusanyika kuusikiliza uongozi wa kata yao ya Ikuna mkoani Njombe nje ya kanisa hilo.
Mchungaji wa kanisa la kilutheli la KKKT Matiganjora Elly Sanga akisema neno juu ya tukio lililotokea la mafuriko hayo.
Hapa uongozi wa kata ya Ikuna umeenda kushuhudia nyumba za wananchi waliokumbwa na maafa hayo.
Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Usharika wa Matiganjora na Nyumba Mbili za Wananchi Katika Kijiji Cha Matiganjroa Wilayani Njombe Zimeezuliwa Kufuatia Mvua Kubwa Ilionyesha na Kuambatana na Upepo Mkali.
Aidha Mvua Hizo Pia Zimesababisha Hasara Kubwa Kwa Kanisa Hilo Kutokana na Kuharibu Ofisi za Kanisa Pamoja na Kuharibu Mazao ya Wananchi na Paa za Nyumba Zao.
Kutokana na Hali Hiyo Diwani wa Kata ya Ikuna Bw Valentino Hongoli Amewataka Wananchi Kuunganisha Nguvu Zao Ili Kukarabati Majengo Hayo Yalioharibiwa na Mvua Hizo Zilizonyesha Feb 21 Mwaka Huu.
Job Fute ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Ikuna Akiwa Kwenye Eneo Hilo Anakemea Tabia ya Baadhi ya Wananchi Kuhusisha Matukio Hayo na Imani za Kishirikina na Kusema Kuwa Kila Mmoja Anapaswa Kushiriki Katika Ujenzi wa Majengo Hayo
Nao Baadhi ya Wananchi Wameushukuru Uongozi wa Kata Hiyo Kwa Kushirikiana Nao Katika Kusaidia Wale Waliopatwa na Maafa Hayo na Hivyo Kuahidi Kuchangia Kwa Kila Kinachohitajika Ili Kufanikisha Ujenzi wa Kanisa na Nyumba Nyingine Zilizoharibiwa
No comments:
Post a Comment