MUHASHAMU ASKOFU ALFRED MALUMA JIMBO LA NJOMBE LEO AMEONGOZA MISA YA IJUMAA KUU AMBAPO JANA ALIONGOZA MISA YA ALHAMISI KUU
Mhashamu Askofu Wa Kanisa Katholiki Jimbo La Njombe Alfred Maluma Amewataka Wakristo Kudumisha Upendo Katika Kipindi Cha Skukuu Na Kuwa Na Roho Ya Kujitoa Katika Kusaidia Wasiyojiweza ,Kutemkbelea Wagonjwa Na Kwenye Huduma Za Kiroho Ili Kuonesha Upendo Na Ukristo Kwa Jamii Yote.
Akizungumza Wakati Akiongoza Misa Ya Siku Ya Maadhimisho Ya Alhamisi Kuu Muhashamu Askofu Maluma Amesema Katika Injili Iliyosoma Siku Ya Jana Yesu Kristu Anawaosha Mitume Na Kusisitiza Huduma Ya Upendo Kwa Mapadre,Wakristo Na Watu Wengine Ambao Kristo Amewakusanya Ili Wapate Huduma Ya Mungu.
Aidha Askofu Maluma Amesema Kuna Umuhimu Wa Mapadre Kuwepo Katika Kanisa Kwamba Ni Kristo Mwingine Ambapo Siku Hiyo Ya Alhamisi Kuu Ni Skukuu Ya Mapadre Ambayo Inaambatana Na Kutoa Huduma Ya Kutakasa Inayoweza Kuambatana Na Huduma Nyingine Za Kibinadamu Kwaajili Ya Kukamilisha Na Kutafsili Sura Halisi Ya Upenda.
Muhashamu Askofu Maluma Amesema Mapadre Kwa Siku Za Alhamisi Kuu Wanatakiwa Kuwa Katika Maeneo Yao Ya Kutolea Huduma Za Kiroho Kwa Waumini Na Kutoa Huduma Ya Kutakasa Ya Sakramenti Ya Wokovu Ambapo Amesema Kigango Ambacho Padre Yupo Maendeleo Yatakuwepo Kutokana Na Moyo Wito Wa Kuarika Watu Waamini Uwepo Wa Kristo.
Hata Hivyo Askofu Huyo Amewaomba Wakristo Kuthamini Mapadre,Kuthamini Kanisa Na Mafumbo Mbalimbali Ili Kuleta Wokovu Huku Wakitakiwa Kuwaombea Mapadre Wote Wafanye Kazi Vizuri Na Kutaka Mapadre Nao Wawe Wanyenyekevu Kila Siku Na Watambuwe Kwamba Wanabemba Dhamana Ya Kanisa.
No comments:
Post a Comment