Mkuu
wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akiwa amembeba mtoto
aliyezaliwa katika Hopsitali ya Wilaya (Dk. Jakaya Kikwete) wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani kiwilaya.
Mkuu
wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Talaba akimpa msaada
mmoja wa mama anayeuguza mtoto katika hopsitali ya wilaya.
Mkuu
wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akizungumza na wauguzi (hawapo
pichani) katika sikukuu ya Wauguzi Duniani viwanja vya hospitali ya
wilaya.
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akitoa neno kumkaribisha mgeni rasmi mkuu wa wilaya
Wauguzi wakila kiapo cha utii wakati wa sikukuu hiyo.
Wauguzi
wilayani Kishapu wamepongezwa kwa kazi nzuri na kutakiwa kuendelea
kuipenda kazi yao kuchapa kazi katika mazingira yoyote waliopo kwani wao
ni chachu ya afya katika jamii.
Hayo
yamesemwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga
Talaba wakati kwenye kilele cha Siku ya Wauguzi Duniani iliyofanyika
katika viwanja vya Hospitali ya Wilaya ya DK. Jakaya Kikwete.
Talaba
ambaye aliwaongoza wauguzi hao na watumishi wa halmashauri kutoa
misaada na kufariji wagonjwa hospitalini hapo aliwapongeza kwa huduma
nzuri kwa wagonjwa.
Alisema
kuwa bila ya wauguzi afya haijakamilika na kuwa uuguzi ni zaidi ya wito
na ni huduma inayohitaji upendo na huruma kwa wale unaowahudumia.
“Kama
huna upendo na ukarimu basi wewe siyo muuguzi na ukionesha ukarimu na
upendo ndiyo mwanzo wa kupona kwa mgonjwa ukifika tu pale mgonjwa
anapona hata kabla hujampa dawa,” alisisitiza.
Aidha,
aliwataka wauguzi waendelee kuwa na ushirikiano baina yao huku
akiwapongeza kwa mafanikio katika sekta ya afya pamoja na kuwa wana
changamoto ya mazingira ya kazi.
Mkuu
huyo wa wilaya aliwaomba kuendelea kutimiza wajibu na kuzingatia viapo
vyao vya uuguzi na kanuni za utumishi huku akionya kushindwa kufanya
hivyo ni kukiuka taratibu za kazi na hivyo kutengeneza migogoro isiyo ya
lazima.
Kwa
upande wake, Kaimu Muuguzi Mkuu Hospitali ya wilaya hiyo ya Dk. Jakaya
Kikwete, Rehema Jumanne akisoma risala alitaja mafanikio yaliyopatikana
kuwa ni mafunzo kazini.Alisema
mafunzo hayo yamesaidia wauguzi kuboresha huduma za jamii zikiwemo
uzazi wa mpango, huduma za dharura kwa wajawazito na kusaidia wachanga
kupumua.
Pia
alitaja mafanikio mengine ni kuendeleza wauguzi katika ngazi za juu za
elimu na hivyo kutoa huduma kwa kiwango cha juu pamoja na kutoa huduma
bora tofauti na mazingira yao.
Hata
hivyo alisema kuna changamoto ya uhaba wa watumishi hiyo husababisha
kutokuwepo kwa uwiano sawia wa watumishi katika kutoa huduma katika
vituo vya afya na zahanati mbalimbali katika wilaya hiyo.
Siku
ya Wauguzi Duniani huadhimisha kila Mei 12 ikiwa ni kumuenzi muuguzi
mwanzilishi Florance Nightingale aliyoanzisha mwaka 1844 ambapo
kaulimbiu ni Wauguzi, mbiu ya kuyafikia malengo endelevu ya millennia.
No comments:
Post a Comment