Saturday, May 13, 2017
WANANCHI WA KIJIJI CHA LWANGU NA NGARANGA WALIA NA BARABARA
MILIONI TISINI ZINADAIWA TAYARI ZIMEKWISHA TOLEWA KWAAJILI YA UTENGENEZAJI WA BARABARA HII HATA MAGARI YANASHINDWA KUPISHANA
HII NI BARABARA YA KUTOKEA LWANGU KWENDA KATA YA IWUNGIRO MJINI NJOMBE
MAKARAVATI YAMEWEKWA KWAAJILI YA KUPITISHA MAJI LAKINI MITARO HAIJATENGENEZWA MAJI YANAKOSA KWA KUPITA TAZAMA KAMA HAPA
NJOMBE
Wananchi Wa Vijiji Vya Lwangu Na Iwungilo Wilayani Njombe Wamelalamikia Kuwepo Kwa Tatizo La Uharibifu Wa Barabara Ambayo Imedaiwa Kutengenezwa Chini Ya Kiwango Kutokana Na Kutotimia Kwa Mita Saba Zinazoweza Kusaidia Magari Kupishana Kwa Uhuru.
Wakizungumza Wakiwa Kwenye Barabara Hiyo Wananchi Wa Vijiji Hivyo Wamesema Barabara Hiyo Imetengenezwa Chini Ya Kiwango Kutokana Na Kutengenezwa Bila Kuzingatia Viwango Vinavyotakiwa Kwa Kuwangalia Upana,Uwekaji Makaravati Na Kutowekwa Mitaro Ya Maji.
Wamesema Kuwa Wamekuwa Wakikabiliwa Na Changamoto Ya Kushindwa Kusafirisha Mazao Yao Ya Viazi Na Mbao Ambapo Wameomba Serikali Kutengeneza Kwa Kiwango Kinachostahili Ili Isiharibike Kwa Muda Mfupi Kama Ambavvyo Imetengenezwa Kwa Sasa Huku Wakikanusha Hoja Ya Kwamba Wananchi Hawataki Kuondoa Miti Iliyopo Kando Ya Barabara Kwani Wako Tayari Kuiondoa .
Mwenyekiti Wa Serikali Ya Utengula Amesema Kuwa Wamekuwa Wakifuatilia Utengenezaji Wa Barabara Hiyo Kwa Mkandarasi Aliyepewa Kazi Hiyo Ambapo Mkandarasi Amewaambia Anatengeneza Kutoka Na Aliyemuajiri Anavyotaka Na Kusema Kuwa Kwa Sasa Barabara Hiyo Haifai Kwa Matumizi.
Diwani Wa Kata Ya Iwungiro Regnad Danda Amekili Kutengenezwa Chini Ya Kiwango Kwa Barabara Hiyo Na Kusema Kuwa Haijafikia Upana Wa Mita Saba Zinazotakiwa Kwenye Utengenezaji Wa Barabara Ambapo Tatizo Hilo Amekwisha Lifikisha Halmashauri Kwaajili Ya Kuboresha Zaidi Huku Akisema Usimamizi Wa Kitaalamu Kutoka Halmashauri Ukiwa Mdogo.
Naye Mkandarasi Anayejenga Barabara Hiyo Wa Kutokea Kampuni Ya SJM Construction co,LTD Kutoka Mafinga Wilayani Mufindi Bwana Samwel Masasi Amesema Barabara Hiyo Bado Hajaikabidhi Kwa Halmashauri Ambapo Anatarajia Kuendelea Kuikamilisha Baada Ya Wiki Mbili Kwa Kupanua Zaidi Ili Iwe Na Kiwango Kinachostahili Huku Akisema Matengenezo Yamefanyika Kwa Hela Aliyopewa.
Kwa Mujibu Wa Mkandarasi Huyo Barabara Hiyo Imedaiwa Inatengenezwa Kwa Gharama Ya Shilingi Milioni Mia 234 Ambapo Hdi Sasa Shilingi Milioni Tisini Zimekwisha Tolewa Na Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Kwaajili Ya Matengenezo Yaliyofanyika Huku Akisema Alisimamisha Kazi Hiyo Kutokana Na Mvua Kuanza Kunyesha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment