Vurugu imetokea leo wakati kundi la watu wanaodaiwa kuwa wanachama wa chama kimoja cha siasa (jina kapuni hadi itapothibitishwa) kupambana na wenzao wanaosadikiwa kuwa wapinzani wao baada ya kundi moja kuvamia mkutano wa upande mmoja na waandishi wa habari katika Hotel ya Vinna Hotel maeneo ya Mabibo jijini Dar es salaam, na kuzua taharuki kubwa kwa waandishi wa habari na wakaazi wa eneo hilo.
Mashuhuda
wamesema watu kadhaa wasiojulikana walifika hapo wakiwa wamefunika
nyuso zao kwa vitambaa huku wakiwa na silaha za jadi na kuanza vurugu.
Baada
ya mkutano kuvurugika baadhi ya waliokuja kufanya vurugu walikimbia
huku wakikimbizwa na wanachi wenye hasira kali ambao walifanikiwa
kumkamata mmoja wao na kumjeruhi kwa kumkata maungio ya kisigino ya
mguu wake wa kulia.
Juhudi za kuwapata wasemaji wa pande mbili hizo zinaendelea.
Taharuki katika Hotel ya Vinna maeneo ya Mabibo jijini Dar es salaam
Mmoja wa watuhumiwa wa uvamizi huo akiwa anapambana
Mmoja wa watuhumiwa wa uvamizi huo akiwa anapambana
Mmoja
wa watuhumiwa wa uvamizi akiwa chini ya ulinzi mara baada ya
kudhibitiwa na na wananchi kisha kumkata mguu na kushindwa kutembea
Mtuhumiwa akiwa amekatwa mguu wa kulia akiugulia maumivu baada ya kujeruhiwa
No comments:
Post a Comment