MKUU WA WILAYA YA NJOMBE B.LUTH MSAFIRI AKIWA KWENYE MAOMBI KANISANI
BI. MSAFIRI HAPA ANAWASALIMIA WAUMINI WA KANISA LA TAG MELINZE
HAPA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE LUTH MSAFIRI ANAMTAMBURISHA MTOTO WAKE WA MWISHO AMBAYE ALIONGOZANA NAE KANISANI HAPO
NJOMBE
Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Bi.Luth Msafiri Amewashukuru Wananchi Kwa Kushiriki Katika Shughuli Mbalimbali Za Kuinua Uchumi Wao Wakiwemo Wakulima Wa Zao La Viazi Ambapo Juhudi Hizo Zitawatia Moyo Na Wananchi Wengine Wasiyojishughulisha Kushiliki Kwenye Miradi Ya Uchumi.
Akizungumza Akiwa Kwenye Ibada Katika Kanisa La Tanzania Assembles Of God La Melinze Mkuu Huyo Wa Wilaya Bi. Msafiri Amepongeza Shughuli Zinazofanywa Na Akina Mama Wa Kanisa Hilo Kwa Kufanya Kazi Ambapo Amesema Hawana Budi Kumshukuru Mungu Kwa Mafanikio Walio Nayo.
B. Msafiri Amesema Njombe Wamebahatika Kuwa Na Mvua Za Kutosha Na Mazao Ya Aina Mbalimbali Yanastawi Na Hivyo Wachungaji Na Viongozi Wanatakiwa Kuwatia Moyo Wakristo Wote Kufanya Kazi Kwa Bidii Kwa Manufaa Yao Huku Akiomba Kuonesha Upendo Kwa Kila Mmoja.
Kwa Upande Wake Mchungaji Wa Kanisa La TAG Melinze Cefania Tweve Amemshukuru Mkuu Wa Wilaya Kwa Kutoa Ushauri Na Kushiriki Pamoja Ibada Hiyo Ambapo Amesema Waumini Wanatakiwa Kuacha Chuki Na Kwamba Nyota Zao Zitang'ara Kwa Kutenda Mambo Mema.
Mchungaji Tweve Amesema Kumekuwa Na Vita Mbalimbali Za Kiroho Ambazo Zinawakabili Wakristo Wakiwa Nyumbani Kwao Na Kusema Maneno Ya Uongo , Tamaa Za Mwili Wanatakiwa Kuacha Ili Nyota Zao Zing'are Kama Somo La Nyota Njema Linavyosema.
Wakati Huo Huo Muhashamu Askofu Wa Kanisa Katholiki Jimbo La Njombe Alfred Maluma Ameongoza Misa Takatifu Ya Skukuu Ya Matawi Ambapo Ametoa Ujumbe Kwa Waumini Wa Kanisa Hilo Kwamba Wanatakiwa Kuzingatia Kanuni Za Kufunga Siku Ya Jumatano Kuu,Alhamisi Kuu, Ijumaa Kuu Na Jumamosi Kuu Na Kutowakwaza Watu Katika Kipindi Hiki Cha Kwaresma.
No comments:
Post a Comment