DIWANI WA KATA YA NJOMBE MJINI AGREY MTAMBO AKIZUNGUMZA NA WANANCHI AKIWA KWENYE ZIARA YA KUTEMBELEA WANANCHI WA KATA HIYO
MJUMBE WA SERIKALI YA MTAA WA BUGURUNI ANTONY MTEWELE AKITETA JAMBO NA DIWANI WA KATA YA NJOMBE MJINI AGREY MTAMBO
WANANCHI WAKIHOJI MASWALI MBALIMBALI HUKU WENGINE WAKIPONGEZA KWA WAZO HILO LA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI
HOSPITALI ILIYOPO MTAA WA SIDO INAYOJENGWA NA WANANCHI WA MITAA MIWILI SIDO NA BUGURUNI IMESHINDWA KUKAMILIKA KWA TAKRIBANI MIAKA 10 FEDHA ZA MICHANGO YA WANANCHI HAZIELEWEKI ZINAKOKWENDA
NJOMBE
Wananchi Wa Kata Ya Njombe Mjini Wametakiwa Kuepukana Na Itikadi Za Siasa Wakati Wa Kutekeleza Miradi Ya Maendeleo Kwenye Mitaa Yao Ambapo Kwa Atakayebainika Anakwamisha Maendeleo Afisa Maafisa Watendaji Wanatakiwa Kuchukua Hatua Dhidi Ya Watu Hao.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Diwani Wa Kata Ya Njombe Mjini Agrey Mtambo Wakati Akizungumza Na Wananchi Kwenye Kata Hiyo Na Kusema Kuwa Yeye Hatakuwa Na Tatizo Endapo Wananchi Wote Watashikamana Kuhakikisha Wanasukuma Miradi Ya Maendeleo Kwa Manufaa Ya Jamii Nzima .
Bwana Mtambo Amesema Kuwa Kwenye Maendeleo Hakuhiytaji Itikadi Za Vyama Vyovyote Vya Siasa Kwani Asiye Na Chama Na Wenye Chama Huduma Zinatolewa Sawa Ambapo Amekemea Baadhi Ya Watu Wanaotumia Mwanya Wa Vyama Vyao Kuzuia Wananchi Wasichangia Miradi Ya Maendeleo Katika Maeneo Yao.
Katika Hatua Nyingine Diwani Mtambo Amewaagiza Watendaji Wa Mitaa Yote Kuhakikisha Wana washughilikia Watakaokwenda Kinyume Na Mipango Ya Serikali Za Mitaa Kwani Yeye Kama Mtendaji Ni Mtumishi Anahitajika Kutofungamana Na Upande Wowote Wa Kisiasa Huku Wananchi Wakiomba Kuwashughulikia Wenye Kwa Madai Mtendaji Atashindwa Kutekeleza.
Kwa Upande Wake Wananchi Wa Mtaa Wa Buguruni Mjini Njombe Wameonesha Kutoakuwa Na Imani Na Afisa Mtendaji Wa Mtaa Wa Buguruni Kwamba Hataweza Kuwashughulikia Baadhi Ya Wanasiasa Wanaozuia Baadhi Ya Wananchi Wasichangie Michango Ya Utekelezaji Wa Miradi Ya Mtaa Kutokana Na Kumezwa Na Chama Kinachoshawishi Wasichangie Ambapo Ameombwa Kufanya Kazi Iliyopeleka.
Katika Hatua Nyingine Serikali Bado Imeendelea Kusisitiza Zuio La Uchinjaji Nguruwe Hadi Serikali Itakapotangaza Kuruhusu Uchinjaji Huo Ambapo Imedaiwa Kuna Baadhi Ya Wachinjaji Wanaendelea Kukaidi Katazo Hilo Nakwamba Watakapobainika Hatua Kali Za Kisheria Watachukuliwa Hatua Kali Za Kisheria.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Afisa Mtendaji Wa Kata Ya Njombe Mjini Bonasius Mwalongo Wakati Akitoa Elimu Na Dalili Za Ugonjwa Wa Homa Ya Nguruwe Kwa Wananchi Wa Mtaa Wa Buguruni Kwamba Nguruwe Anakosa Nguvu Za Kusimama Kutokana Na Kukosa Nguvu Miguu Ya Nyuma.
Bwana Mwalongo Amesema Kwa Sasa Nyama Ya Nguruwe Inayouzwa Kwa Kificho Wameipatia Jina La Mchicha Pasipo Wachinajaji Hao Kufahamu Madhara Yake Ambapo Ameomba Wananchi Kutoa Taarifa Kwa Viongozi Watakapomuona Mtu Anauza Nyama Ya Nguruwe Kinyume Na Maagizo Hayo.
Katika Hatua Nyingine Bwana Mwalongo Ametaka Wananchi Wanaofuga Mbwa Kufungulia Kuanzia Saa Tano Usiku Wakati Wananchi Wakiwa Wamelala Kwani Endapo Mbwa Watazagaa Hovyo Wanaweza Kusababisha Madhara Ya Kichaa Cha Mbwa Kwa Watakaong'atwa.
Kwa Upande Wake Mjumbe Wa Serikali Ya Mtaa Wa Buguruni Antony Mtewele Amesema Utaratibu Wa Serikali Ya Mtaa Unatakiwa Kufuatwa Kwa Kuepukana Na Vikao Vya Siasa Huku Akitaka Taarifa Za Kuzagaa Kwa Mbwa Zitolewe Ofisini Ili Hatua Zichukuliwe Za Kuua Mbwa Hao.
Diwani Wa Kata Ya Njombe Mjini Agrey Mtambo Leo Amehitimisha Ziara Yake Kwa Kutembelea Mitaa Tisa Ya Kata Ya Njombe Mjini Ambapo Amejibu Maswali Mbalimbali Kwa Wananchi Kuhusiana Na Changamoto Zilizokuwa Zinawakabili Na Zinahitaji Majibu.
No comments:
Post a Comment