MADIWANI WALIOPEWA SEMINA YA SIKU MBILI WAKIBADILISHANA JAMBO NA MKUU WA WILAYA YA LUDEWA ANDREA TSERE MWENYE SUTI NYEUSI
NJOMBE
Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Christopha Ole Sendeka Amepongeza Madiwani Waliohudhuria Semina Ya Siku Mbili Na Kusema Kuwa Mafunzo Hayo Wanatakiwa Kuyatumia Kikamilifu Katika Maeneo Yao Ambapo Elimu Walioipata Inatakiwa Kwenda Kutatua Changamoto Kwa Wananchi.
Akizungumza Kwa Niaba Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe, Mkuu Wa Wilaya Ya Ludewa Andrea Tsere Amesema Semina Hiyo Ina Umuhimu Mkubwa Kwani Kuwaelimisha Madiwani Ni Kuunganisha Wananchi Na Serikali Yao Kwa Kuwa Ndiyo Wanaowawakilisha Wananchi.
Tsere Amesema Maendeleo Ya Nchi Hayatekelezwi Na Serikali Kuu Peke Yake Badala Yake Yananzia Kwenye Shina La Maendeleo Ambalo Ni Ngazi Ya Kata Watakao elimisha Viongozi Wa Vijiji Kwaajili Ya Kupata Miradi Na Maadili Yalio Mema Ambapo Sasa Watakidhi Mahitaji Ya Serikali Za Mitaa.
Bwana Tsere Amesihi Madiwani Wote Kuwa Na Maadili Katika Kusimamia Rasmali Mbalimbali Za Wananchi Ikiwemo Fedha , Miradi Ya Magari Na Ujenzi Wa Miundombinu Inayojengwa Kwenye Vijiji Na Kata Pamoja Na Kukataa Kupokea Na Kutoa Rushwa .
Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Bi.Luth Msafiri Amepongeza Waandaaji Wa Semina Hiyo Ya Kuwajengea Uwezo Madiwani Ambapo Amewasihi Kwenda Kuyatumia Kikamilifu Na Kuzingatia Maadili Kwa Wananchi Wakati Wa Kutekeleza Miradi.
Baadhi Ya Washiriki Wa Semina Hiyo Wameshukuru Kwa Elimu Waliyopewa Ambapo Kupitia Semina Hiyo Wamepata Elimu Kubwa Itakayotumika Kuwaongoza Wananchi Katika Maeneo Yao Ya Utawala.
Mafunzo Hayo Yameandaliwa Na Mradi Wa Kuimarisha Mifumo Kwa Sekta Za Umma Unaofadhiliwa Na Marekani USAID.
No comments:
Post a Comment