Monday, February 13, 2017
WILAYA YA NJOMBE YAPINGA UKATILI KWA WATOTO WA KIKE
NJOMBE
Jamii Imetakiwa kuepukana na Tabia za Ukatili wa Kijinsia kwa watoto na ukatili unaomnyanyasa Mwanamke ambapo Kesi kama Hizo zinatakiwa kupelekwa katika Dawati la Kijinsia Linalosimamiwa na Jeshi la Polisi Pamoja na Ofisi ya Ustawi wa Jamii katika Halmashauri husika ili kupunguza tabia hizo kwa baadhi ya ya Wazazi Wilayani Njombe.
Rai Hiyo imetolewa na Afisa Ustawi wa Jamii Katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Averino Chaula wakati akizungumza na Uplands Fm Kuhusiana na Juhudi za Kupinga Ukeketaji kwa watoto wa Kike ambalo linaendelea kwa Wananchi katika baadhi ya mikoa iliyopo Hapa Nchini.
Bwana Chaula amesema Ukeketaji Kwa Watoto wa Kike ni aina mojawapo ya Ukatili wa Kijinsia na kwamba kuna aina tano za Ukatili Ikiwemo Mila na destuli zinazoruhusu Ukeketaji, Ukatili wa Kingono ,Ukatili wa Kimwili, Ndoa za Utotoni,Ukatili wa Kihisia ,Utelekezaji watoto na Ukatili wa Kiimani ambapo kwa Njombe kesi za Ukeketaji hazipo na zilizopo ni zile za ukatili wa Kimwili na Ubakaji ambao Asilimia Zinazidi Kupanda kwa asilimia 54.
Amesema Wananchi wanatakiwa kupinga Tabia za Ukatili wa Kijinsia kwa watoto wa Kike ambapo elimu imekuwa ikiendelea kutolewa kwa Wananchi juu ya Madhara ya Ukatili nakuzitaka timu za Kupambana na Kuzuia Tabia za Ukatili kuanzia Ngazi za Vijiji Na Kata kutilia Mkazo tatizo hilo lisijitokeze eneo lolote la Wilaya ya Njombe na Kuonesha Ushirikiano katika Kutoa Taarifa Watakapoona Kuna Vitendo hivyo Kwa Baadhi ya Maeneo.
Wakizungumza kwa Nyakati Tofauti Baadhi ya Wananchi Mjini Njombe Wameomba Hatua kali za kisheria Kuchukuliwa dhidi ya wanaotelekeza watoto na Kuwafanyia Vitendo vya Ukatili ambapo wametupia Lawama Vyombo vinavyosimamia sheria za Ukatili kwa Kushindwa kutoa adhabu kali kuwa mfano kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment