Monday, February 13, 2017
ASA YAJIPANGA KUWAFIKIA WAKULIMA KUWAUZIA MBEGU ZA MAHINDI
NJOMBE
Wakala wa Serikali wa Mbegu kutoka Mikoa ya Nyanda za juu kusini kituo Cha Njombe ASA Wamefanikiwa kuuza Mbegu za Mahindi ya Muda Mfupi wa Miezi mitatu OPV Na zile Za Muda Mrefu Highibread Zaidi ya Tani 40 kwa wakulima wa Mikoa mbalimbali ikiwemo ya Njombe na Iringa kwaajili ya kuwasaidia wakulima kupata mavuno yakutosha na yalio bora .
Afisa masoko wa Wakala wa serikali wa Usambazaji Mbegu Nchini Kituo cha Njombe Maria Shishila amesema kituo cha Uzarishaji na Utengenezaji Mbegu cha Njombe Kinatarajia Kutangaza kwenye Vyombo Vya Habari ,Vipeperushi ,mikutano mbalimbali na kuwafikia baadhi ya wakulima kutoa Elimu Juu ya Kuzitumia Mbegu za ASA zinazoandaliwa na Serikali Kumukomboa Mkulima Wa zao la Mahindi.
Bi.Shishila Amesema kutokana na mwakajana wakala huyo Kuuza Mbegu zaidi ya Tani 40 mwaka Huu wanatarajia kuuza Zaidi ya Tani 70 ya mbegu zinazozalishwa katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya nyanda za juu kusini na kufanyiwa utafiti na serikali Ambapo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kuzitumia kwaali ya kuongeza mavuno katika mashamba yao.
Christopha Daffa ni Afisa Kilimo Wa Wakala Huyo Wa ASA Amesema mbegu hizo zinachukuliwa kwenye mashamba ya magereza , Mashamba ya Majeshi yaliopo mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na kuzitengeneza kwenye Kituo cha Njombe Ambapo amewatoa Hofu wananchi juu ya Ubora wa Mbegu hizo kwamba mbegu hizo zimefanyiwa utafiti kwaajili ya kilimo cha Mikoa ya Nyanda za Juu kusini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment