MADIWANI WAKIJADILI RASMI HIYO ILIYOPITISHWA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 41
KAIM MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE AKIZUNGUMZA
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE LUTH MSAFIRI AKIZUNGUMZA NA MADIWANI KWAAJILI YA KUCHANGIA HOJA
DIWANI WA KATA YA RAMADHANI GEOGE MENSON SANGA AKICHANGIA HOJI ZA BAJETI HIYO
HAWA NI MADIWANI WA HALMASHAURI YA MJI WA MJI WA NJOMBE WAKIWA KWENYE KIKAO HICHO
DIWANI WA KATA YA NJOMBE MJINI AGREY MTAMBO AKIZUNGUMZA KWENYE BARAZA HILO
NJOMBE
Halmashauri ya Mji wa Njombe imepitisha rasimu ya Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2017/2018 zaidi ya shilingi bilioni 41 kutoka vyanzo mbalimbali ikiwa ni mapato ya ndani na Ruzuku toka serikali Kuu ambapo mapato ya ndani ni zaidi ya shilingi bilioni 3,Ruzuku toka serikali kuu ni zaidi ya shilingi bilioni 33 na Fedha kutoka kwa Wahisani ni zaidi ya shilingi bilioni 5.
Akisoma taarifa ya mapendekezo ya rasimu ya Bajeti hiyo Mchumi na Afisa Mipango wa halmashauri hiyo Filbert Mbwiro amesema kwa mwaka wa fedha uliopita Halmashauri imefanikiwa kupokea na kukusanya zaidi ya shilingi Bilioni 11 sawa na asilimia 31.1 ya lengo la zaidi ya shilingi bilioni 35 kutoka Vyanzo mbalimbali vya mapato imetumia zaidi ya shilingi Bilioni 8 sawa na asilimia 75.6 ya makusanya kwa bajeti iliyoidhinishwa .
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Maalumu wa Baraza kuu la madiwani kwaajili ya Kujadili Rasimu ya Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2017/2018 mwenyekiti wa halmashauri Hiyo Edwin Mwanzinga amehimiza Madiwani kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato ili halmashauri hiyo iweze kujiendesha yenyewe kupitia mapato ya ndani.
Mwanzinga amesema kuwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 bajeti ya Halmashauri ya mji Inapaswa kulenga kukamilisha miradi ambayo haijakamilika ili iweze kuanza kutoa huduma kwa jamii na thamani ya fedha kuonekana na kusema kuwa miradi mingi ya Halmashauri inatekelezwa kupitia fedha za mapato ya ndani.
Baadhi ya Wajumbe wa mkutano huo wa baraza la madiwani wamehoji upatikanaji wa fedha mbalimbali zinazotoka kwenye vyanzo vya mapato kama ziko sahihi ikiwemo makusanyo yaliopo njiapanda ya magereza,Soko kuu la Njombe Mjini na soko la Joshoni kutotumika kwa muda mrefu ikiwa limekwisha kamilika .
Mapato ya ndani hadi kufikia Mwezi Decemba 2016 halmashauri ya mji imekusanya Zaidi ya shilingi bilioni 1 sawa na asilimia 50 ya lengo la kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 2 ambapo madiwani wanatakiwa kuwa kitu kimoja katika kukusanya mapato kwaajili ya Halmashauri.
No comments:
Post a Comment