Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, February 12, 2017

JIKUMBUSHE MAADHIMISHO YA KUTIMIZA MIAKA 40 YA KUZALIWA KWA CCM



 MWENYEKITI CCM  MKOA WA NJOMBE DEO SANGA  AKIWA NA VIONGOZI WENGINE WA CHAMA PAMOJA NA SPIKA MSATAAFU WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ANNE MAKINDA NA MKUU WA MKOA WA NJOMBE CHRISTOPHA OLE SENDEKA





 
































































 NJOMBE

Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe  Kimewataka Watumishi Mbalimbali Serikalini Kuzingatia Kanuni na Maadili ya Utumishi wa Umma Katika Kutekeleza Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2015/2020.

Agizo Hilo Limetolewa na Mwenyekiti wa Chama Hicho Mkoa Bwana Deo Sanga Ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Makambako Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 40 ya Kuzaliwa Kwa Chama Hicho Yaliyofanyika Kimkoa na Kiwilaya Mjini Makambako.

Mwenyekiti Sanga Pia Amemuomba Mkuu Wa Mkoa Kufuatilia na kusimamia Upimaji wa Ardhi na Utoaji Hati Miliki Za Ardhi kwa Wananchi Wa Mkoa huo Ili kuondokana na Migogoro ya Ardhi inayoendelea kuwakabili baadhi ya wananchi  Ili Waweze Kuwa na Uhakika wa Umiliki wa Ardhi Itakayowasaidia Kupatiwa Mikopo  Kwenye Taasisi Mbalimbali za Fedha.


Bi. Anne Makinda ni Spika Mstaafu  wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Nne Ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Bima ya Afya Taifa Ametumia Maadhimisho Hayo Kuwaasa viongozi waliotokana na CCM kuepukana na tabia za kuomba Rushwa Kwa Wananchi,Kuacha kupata fedha kwa njia ya Udanganyifu,kuwa wakweli ili kujenga CCM Mpya na Tanzania Mpya.

Aidha Spika Mstaafu Makinda Amepongeza Uongozi wa Mkoa wa Njombe Kwa Kufanikisha Kushika Nafasi ya kwanza Kitaifa Katika Matokeo ya Mtihani wa Kidato Cha Nne Kwa Mwaka Uliopita Kwani Hatua Hiyo ni Nzuri Katika Maendeleo ya Taifa.

Kwa Upande Wake Katibu Wa CCM Mkoa wa Njombe  Hosea Mpagike Amesema Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Kimefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali  ya maendeleo ikiwemo kujenga Ofisi ya Chama ya  Mkoa
 iliyopo Mtaa wa Mjimwema Mjini Njombe Huku Katibu Wa CCM Wilaya Sadakati Kimatti Akisema katika Kuadhimisha Miaka 40 ya kuzaliwa kwa chama hicho  Wamefanikiwa Kutembelea na kupanda miti katika kata ya Utengule mjini Makambako.


Edward Mgaya Ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya  ya Njombe  Ambaye Amewapongeza Wanachama kwa Mshikamano Uliopo Kwa Sasa ambapo amesisitiza Kuondoa tofauti zao katika Chama badala yake wadumishe Mshikamano  na kwamba kwa atakayeona hawezi kushirikiana na wanachama wa CCM Anaweza kuachia ngazi kuliko kuvulugha Chama.

Februari 5 ya Mwaka 1977 Ndio Tarehe Kilipoasisiwa Chama Hicho Chini ya Muasisi Wake Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Ambapo Miongoni Mwa Mambo Makubwa Ambayo Chama Hiki Kitajivunia ni Kuendelea Kushika Dola Tangu Kupatikana Kwa Uhuru wa Tanzania Mwaka 1961 Hadi Sasa.

















































No comments:

Post a Comment