MKUU WA WILAYA YA NJOMBE LUTH MSAFIRI AKIPANDA MTI KUTEKELEZA ZOEZI LA UZINDUZI KATIKA ENEO LA SHULE YA MSINGI NYOMBO KATA YA IKUNA
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AKISAINI KITABU KABLA YA KUFANYA UZINDUZI WA ZOEZI LA UPANDAJI WA MITI
WANAFUNZI NA WANANCHI WAKIWA KATIKA HARAKATI ZA UPANDAJI MITI
MWENYEKITI WA HALMSHAURI YA WILAYA YA NJOMBE VALENTINO HONGORI AKIPANDA MTI
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE MONICA PZ KWILUHYA NAE AKIWA KATIKA ZOEZI LA UPANDAJI WA MITI KWENYE UZINDUZI WA ZOEZI LA UPANDAJI MITI KIWILAYA
NJOMBE
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Luth Msafiri leo Amezindua Zoezi la Upandaji wa Miti katika Halmashauri ya Wilaya hiyo ambapo jumla ya Miti aina ya Mikaratus Elfu Moja Imepandwa kwenye shamba la shule ya msingi Nyombo lenye ukubwa wa ekari 2.24 .
Akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Nyombo Bi.Msafiri ametaka wananchi kuacha kupanda miti kwa mazoea badala yake wapande kwa lengo la Kibiashara na endelevu kwaajili ya kutunza mazingira kwa kupanda pia miti iliyo rafiki na vyanzo vya maji na kuinua uchumi wa familia zao.
Aidha Bi. Msafiri ametaka taasisi za serikali zinatakiwa kuotesha miche ya miti wenyewe na siyo kununua kwa taasisi nyingine ili na wanafunzi wa eneo husika waweze kujifunza namna ya kuotesha ambapo pia amehimiza ufugaji wa nyuki kuinua uchumi wa kila mmoja.
Awali akisoma Risala Fupi ya Uzinduzi wa Upandaji Miti Kiwilaya Afisa maliasili Wilaya ya Njombe Libenanga Paul amesema Halmashauri hiyo inatarajia kupanda miti zaidi ya milioni 14 ambayo imeoteshwa na taasisi za serikali na za watu binafsi,vikundi na makampuni.
Kwa Upande wake wananchi waliohudhuria uzinduzi huo wameomba serikali kuwapunguzia ushuru wa Mbao ambao umekuwa ukitozwa kwenye mageti huku swala la kuvuna Miti wakitaka Itafutwe Mbinu nyingine ya kuwawezesha wakulima ili wasivune kabla ya kukomaa kwa miti huku wakitaka wasipangiwe muda wa kuvuna kwa kuwa wakati wa kupanda wamepanda kwa hiari yao.
Kauli mbiu ya Maadhimisho hayo inasema BIASHARA YA MITI, PANDA MITI UONGEZE KIPATO CHA FAMILIA NA HIFADHI MAZINGIRA.
No comments:
Post a Comment