HII NI OFISI YA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE AMBAYO IMEKABIDHI MILIONI MIA 106 ZA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA VIJANA NA AKINA MAMA WAJASILIAMALI 51.
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE ILUNATA MWENDA AKITOA MANENO YA UTANGULIZI MBELE YA VIKUNDI HIVYO
MWENYEKITI WA HALMASHAURI AKIKABIDHI HUNDI ZA MIKOPO KWA WANAVIKUNDI NA SACCOS
WANAVIKUNDI WAKIPOKEA HUNDI ZA MIKOPO
B. ALONE NA KIKUNDI CHAKE CHA CLUSC NUMBERED NAE AKIPOKEA HUNDI YA MKOPO
AFISA MAENDELEO YA JAMII BI.YOHANA KALINGA AKIWA KWENYE UKUMBI HUO ULIOTUMIKA KUWAKABIDHI MIKOPO VIJANA NA AKINA MAMA
Halmashauri ya Mji wa Njombe imekabidhi mkopo wa shilingi milioni mia moja na sita kwa vikundi 51 vya wajasiliamali waliopo katika halmashauri hiyo pamoja na Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo SACCOS Zikiwemo Anglikana na Luponde SACCOS.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bi.Iluminata Mwenda akimkaribisha mwenyekiti wa Halmashauri Edwin Mwanzinga kukabidhi Hundi kwa vikundi mbalimbali pamoja na Saccos nane zilizopo katika Halmashauri hiyo na kusema fedha hizo zimetokana na marejesho ya fedha zilizokopeshwa kwa vikundi pamoja na mapato ya ndani .
Bi.Mwenda amesema vikundi na Saccos Hizo zitaendelea kunufaika na Mikopo kutoka kwenye Halmashauri hiyo kulingana na Marejesho ya fedha kutoka kwenye Vikundi kuwa mazuri ambapo fedha hizo zitawanufaisha hata wajasiliamali wengine wa Njombe Mjini.
Akizungumza Mbele ya Wanavikundi na Wawakilishi wa vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo Saccos Mwenyekiti wa Halmashauri Hiyo Edwin Mwanzinga akiwa Mgeni Rasmi amewataka wajasilimali kujitahidi kuwa waaminifu katika zoezi la kuzirejesha fedha hizo za mikopo ili kuendelea kuwanufaisha na wajasiliamali wengine na wao wenyewe.
Mwanzinga amesema kwa kiwango kikubwa Vikundi vya Akina mama vimeonesha Uaminifu Mkubwa katika marejesho ya fedha za mikopo kutoka Halmashauri kuliko Vikundi vya Vijana ambapo ameomba Wasimamizi wa Marejesho hayo kusimamia kikamilifu marejesho na Uaminifu katika Mikopo hiyo.
Kwa Upande wake baadhi ya wajasiliamali Wakizungumza na Uplands Fm wameshukuru kwa Mkopo huo uliotolewa na Halmashauri na kuahidi kurejesha kwa wakati huku wengine wakisema Watashirikiana na Saccos Kikamilifu kuhakikisha mikopo hiyo inawanufaisha nakwamba watakwenda kuwaelimisha Vijana Wengine wajiunge na Vikundi hivyo au kuunda vikundi vingine wanufaike na mikopo hiyo.
Mikopo hiyo imetolewa kwa vikundi vya kata 11 vilivyopo Katika Halmashauri hiyo hiyo ambapo mikopo kama hiyo inatarajia kutolewa tena mwezi april kwa wajasiliamali hao.
.............................................................................................
No comments:
Post a Comment