Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, February 15, 2017

NJOMBE MJI KUCHAPA 3-1 COASTAL UNION YA TANGA KATIKA UWANJA WA AMANI MAKAMBAKO


 WACHEZAJI WALIOKUWA NJE WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA WAKITAKA KUINGIA KUPASHA KIDOGO NDANI YA UWANJA WA AMAN MAKAMBAKO BAADA YA MUDA WA MAPUMZIKO KUFIKA










 MKUU WA MKOA WA NJOMBE CHRISTOPHA OLE SENDEKA AKIKAGUA TIMU KATIKA UWANJA  WA AMANI MAKAMBAKO NA HII NI TIMU YA COASTAL UNION YA TANGA



 HAWA NI WA CHEZAJI WA TIMU YA NJOMBE MJI





 MKUU WA WILAYA YA NJOMBE LUTH MSAFIRI AKIWAO NA MKUU WA MKOA WA NJJOMBE KUSHUHUDIA TIMU YA NJOMBE MJI IKIPAMBANA NA TIMU PINZANI YA COASTAL UNION
  NDEREMO ZA WACHEZAJI WA TIMU YA NJOMBE MJI BAADA YA KUTOKA NA USHINDI WA MAGOLI MATATU KWA MOJA DHIDI YA TIMU YA COASTAL UNION YA  MKOA WA TANGA
 ERASTO MPETE AKIWA JUU KWA KUNYANYULIWA NA WACHEZAJI WA TIMU BAADA YA KUPATA USHINDI WA KISHINDO

Timu ya Mpira wa Miguu ya Njombe Mji imeibuka Kidedea Baada ya Kuicharaza Bao Tatu kwa Moja Timu ya Coastal Union Ya Mkoa Wa Tanga Katika Mchezo uliochezwa Jumapili katika Uwanja wa Amani  Mjini Makambako Mkoani Njombe.

Goli la Kwanza La Timu ya Njombe Mji Lilifungwa Na Mshambuliaji Musa Kipao Kunako Dk ya 16 Ya mchezo huo ambapo Timu ya Njombe Mji Ilikuja Kuwapagawisha Mashabiki Wake Tena Kwa Mara ya Pili Baada ya Musa Ngunda Kuandika Bao la Pili Kunako Dk ya 29.

Katika Kipindi Cha  kwanza Timu hizo Mbili Zilitoka Kwa Kufungana Goli Mbili Kwa Bila ambapo Kipindi cha Pili  Timu Ya Njombe Mji Iliandika Goli la Tatu Kupitia Kwa Mshambuliaji Wake Aden Chepa aliyefunga Katika Kipindi cha Pili  Dk ya 79  baada ya Coastal Union Kuanza Kurudisha Magoli kwa Kuandika Goli la Kwanza.

Coastal Union Ya Tanga Imejipatia Goli la Kwanza Kupitia Mshambuliaji  wake  Ally Mohamed Dk ya 78 ambapo hadi Mchezo unamalizika Njombe Mji walikuwa na Goli Tatu Kwa Moja.

Katika Mchezo Huo Njombe Mji Wakati wa Mchezo mchezaji   Musa Kapao Alipata Kadi Ya Njano Kutokana na Kosa Alilofanya wakati wa Mchezo Huku Wachezaji wa Coastal Union Ya Tanga Wachezaji Wawili Bakary  Nondo Na Mohamed Ally Wakipewa Kadi Za Njano Na Muamuzi.

Timu Ya Njombe Mji Inatarajia Kwenda Kukutana Uso kwa Uso Na Timu Ya Kurugenzi Ya Mafinga Mnamo Tarehe 18 mwezi huu ambayo ndiyo Mechi ya Mwisho Kwa Njombe Mji Kupata Mwafaka Wa Kuapanda Daraja Au Kushuka Daraja .

No comments:

Post a Comment