WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU NCHEMBA AKIZUNGUMZA NA VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA VYA MKOA WA NJOMBE
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AKIWASILI KWENYE UKUMBI WA MKUTANO WA CHUO CHA MAENDELEO
MKUU WA MKOA WA NJOMBE CHRISTOPHA OLE SENDEKA AKIZUNGUMZA KABLA YA KUMKARIBISHA WAZIRI HUYO
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba Ameyataka Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Njombe Kutimiza Wajibu Wake Na Kutimia Nguzo Zote Katika Kupambana na Zoezi la Kutokomeza Matumizi Na Uuzwaji Wa Madawa Ya Kulevya.
Mwigulu Nchemba Amesema Miongoni Mwa Mambo Ambayo Serikali Haitakuwa na Mjadala Nayo Ni Pamoja Na Uharifu wa Kutumia Silaha, Viashilia Hatarishi Vya Ugaidi, Ubakaji Na Mambo mengine yanayohusiana na Hayo kwamba hayana mjadala wowote Watumie Nguvu Zote Kutokomeza Hayo.
Waziri Nchemba Amesema Jambo Lingine Lisilo Na Mjadala Ni swala la Ujangili Ambapo Ametaka Watuhumiwa Ambao Hawana Hatia Waachiliwe Huru Wakiwemo Waendesha Pikipiki Maarufu Kama Bodaboda Na Wengine Ambao Hawana Makosa Yoyote.
Katika Hatua Nyingine Nchemba Amesema Majeshi Ya Magereza Yanatakiwa Yaanze Kujiandaa Na Shughuli Za Kilimo Cha Mazao Ya Chakula Kwa Kutumia Nguvu Kazi Walionayo Na Kusema Kuwa Wanauwezo Wa Kuzarisha Mazao Wakawauzia NRFA,Wakarisha Shule Za Sekondari Na Za Msingi.
Awali Akimkaribisha Waziri Huyo Wa Mambo Ya Ndani Mwigulu Nchemba Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Christopha Ole Sendeka Amesema Kwa Siku Ya Jana Februari 13 Jeshi La Polisi Limefanikiwa Kukamata Dawa Za Kulevya Kilo Nane Za Bangi.
Akiwa Mkoani Njombe Mwigulu Nchemba Ametembelea kambi ya Jeshi la Wananchi Kikosi Namba 347 kilichopo Makambako na Kupanda Nao Miti,Ametembelea Ofisi Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe na Kupokea Taarifa Kwenye Ofisi Ya Kamanda Wa Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe.
No comments:
Post a Comment