WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI LUHUJI B NA A WAKIINGIZA MIFUKO YA SARUJI KWENYE CHUMBA CHA KUHIFADHIA MALI
MWANAFUNZI AKIHESABIA MIFUKO YA SARUJI ILIYOTOLEWA
ADELHELMA MAPUNDA MWALIMU MKUU SHULE YA MSINGI LUHUJI AKIZUNGUMZA BAADA YA KUKABIDHIWA MSAADA HUO
MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI LUHUJI B BENSON THADEO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
DIWANI WA VITI MAALUMU JIMBO LA NJOMBE MJINI ANGELA MWANGENI AKIWA NA KATIBU WA JUMUIYA YA WZAZI YA CCM WILAYA YA NJOMBE
NJOMBE
Diwani wa Viti Maalumu Jimbo la Njombe Mjini Angela Mwangeni Amekabidhi Msaada Wa Mifuko ya Saruji 20 Yenye Thamani ya Shilingi Laki Tatu Kwa Shule Za Msingi Luhuji A Na B Kwaajili ya Kujengea Vyumba Vya Kupikia Chakula Cha Wanafunzi Hao.
Akizungumza Mara Baada Ya Kukabidhi Msaada Huo Kwa Walimu Wakuu Wa Shule Za Msingi Luhuji A Na B Angela Mwangeni Amesema Katika Kutambua Jitihada Zinazofanywa Na Wananchi Za Kutekeleza Miradi ya Shule Amelazimika Kuchangia Kiasi Hicho Cha Mifuko Ya Saruji Kupunguza Mzigo Wa Michango Kwa Wananchi.
Aidha Mwangeni Ametumia Fursa Hiyo Kuwaomba Wadau Wa ELimu Mjini Njombe Kujitokeza Kutoa Misaada Mbalimbali Kwenye Taasisi Za Elimu Zilizopo Karibu Nao Ili Kusaidia Kupunguza Mzigo Wa Michango Ya Utekelezaji Miradi Inayowakabili Wananchi Ya Kujenga Majiko, Vyumba Vya Madarasa Na Mabwalo Ya Chakula.
Adelhelma Mapunda Na Benson Thadeo ni Walimu Wakuu Wa Shule Za Msingi Luhuji A Na B Ambao Wameshukuru Kwa Msaada Huo Uliotolewa Na Diwani Huyo Na Kusema Umepunguza Changamoto Ya Kununua Mifuko Ya Saruji Kwaajili Ya Ujenzi Wa Majiko Ya Shule Na Kuomba Wadau Wengine Kujitokeza Kusaidia Ujenzi Huo Ukiwemo Wa Mabwalo ya Chakula.
Wakizungumza Na Uplands Fm Baadhi Ya Wanafunzi Wa Shule zote Mbili Luhuji A Na B Wameomba Wazazi Kupeleka Michango Mbalimbali Ya Chakula Na Ile Inayohitajika Shuleni Ili Kuondoa Usumbufu Wa Wanafunzi Kuwa Na Hofu Ya Kuyumbishwa Kwa Kurudishwa Nyumbani Badala Ya Kuendelea Na Masomo.
No comments:
Post a Comment