mwenyekiti wa halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Valentino Hongori Akitoa Haotuba Yake Mbele ya Madiwani wa Wilaya.
HAWA NI MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA WAKISIKILIZA KWA UMAKINI
DIWANI WA KATA YA KIDEGEMBYE JULIUS SALINGWA AKICHANGIA HOJA YA ELIMU
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE BI.MONICA KWILUHYA AKIZWAAGIZA WATUMISHI WA MALIASILI KWENDA KUFUKUZA WANYAMA WAHARIBIFU WA MAZAO AINA YA MAHINDI LUPEMBE
NJOMBE
Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Imefanikiwa Kukusanya Shilingi Bilioni 10.048 Hadi Kufikia Mwezi Decemba 2016 Sawa Na Asilimia 48 Ya Lengo La Kukusanya Shilingi Bilioni 21.6 Kutoka Kwenye Vyanzo Mbalimbali Vya Mapato Ya Ndani Ya Halmashauri Hiyo Ambazo Zilikadiliwa Kukusanywa Mwaka Wa Fedha Wa 2016/2017.
Akizungumza Kwenye Mkutao Wa Baraza La Madiwani Mwenyekiti Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Valentino Hongori Amesema Kuwa Hadi Kufikia Decemba 2016 Halmashauri Hiyo Imetumia Shilingi Bilioni 9.6 Sawa Na Asilimia 45 Ya Kutumia Shilingi Bilioni 21.6 .
Bwana Hongori Amesema Kuwa Mwaka Wa Fedha Wa 2016/2017 Halmashauri Ilitenga Shilingi Milioni 7.4 Kwaajili Ya Utekelezaji Wa Miradi Mbalimbali Ambapo Hadi Kufikia Decemba 2016 Jumla Ya Shilingi Bilioni 3.191 Zimepokelewa Kati Ya Shilingi Bilioni 7.4 Sawa Na Asilimia 43.
Hongori Amesema Kuwa Jumla Ya Shilingi Bilioni 2.016 Zimetumika Kutekeleza Miradi Mbalimbali Sawa Na Asilimia 63 Ya Fedha Zilizopokelewa Na Kwamba Asilimia Ndogo Ya Matumizi Imetokana Na Fedha Nyingi Kuwafikia Mwezi Decemba.
Hongori Amewataka Madiwani Wa Halmashauri Hiyo Kusimamia Kikamilifu Mapato Ya Ndani Ili Halmashauri Iweze Kuendeshwa Kwa Kuweka Mikakati Madhubuti Ya Kusimamia Ukusanyaji Wa Maato Huku Akipongeza Kwa Mafanikio Yaliopatikana Katika Kipindi Cha Kufikia Robo Ya Pili Ya Mwaka Walikuwa Wamefanikiwa Kuvukua Asilimia 50 Ya Ukusanyaji Mapato.
Kwa Upande Wake Madiwani Wa Halmashauri Hiyo Wakichangia Mada Mbalimbali Wamesema Kukosekana Kwa Taarifa Kwa Baadhi Ya Kata Kunatokana Na Uzembe Wa Baadhi Ya Watendaji Wa Kata Akiwemo Mtendaji Wa Kata Ya Matembwe Ambaye Ameshindwa Kuandaa Taarifa Kwaajili Ya Baraza Hilo.
No comments:
Post a Comment