Monday, February 27, 2017
BODABODA NJOMBE WAPINGA KODI YA MAEGESHO ,WAKUBALI KULIPA YA SUMATRA
MAAMNDAMANO YA KUSHINIKIZA PIKIPIKI ZILIZOKAMATWA ZIACHIWE NA HAPA WANAELEKEA OFISI ZA UJENZI ZILIKOHIFADHIWA PIKIPIKI AMBAZO ZIMEKAMATWA KWA KUTOLIPA KODI YA SUMATRA.
MADEREVA WANAJADILIANA WAKATI WAKIWASUBILI VIONGOZI WAO WAFIKE ENEO LA TUKIO
KAIMU AFISA SUMATRA MKOA WA NJOMBE DENIES MAGHEMBE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE
NJOMBE
Wamiliki Na Madereva Wa Pikipiki Maarufu Kama Bodaboda Leo Wamefanya Mgomo Wa Takribani Saa Tatu Kushinikiza Viongozi Wa Sumatra Kuziachia Pikipiki Tatu Zilizokamatwa Kutokana na Kushindwa Kulipia Kodi Ya Sumatra Shilingi Elfu 22.
Wakizungumza Wakiwa Kwenye Mgomo Huo Baadhi Ya Madereva Wa Bodaboda Wamesema Kuwa Wanashindwa Kuelewa Serikali Kuwataka Kulipa Kodi Ya Sumatra Ambayo Shilingi Elfu Kumi Inakwenda Halmashauri Na Shilingi Elfu Kumi Na Mbili Inakwenda Makao Makuu Ya Sumatra Huku Halmashauri Ikitoza Kodi Nyingine Shilingi Elfu Kumi Ya Maegesho.
Madereva Hao Wametaka Kupatiwa Ufafanuzi Kuhusiana Na Kodi Ya Maegesho Inayotozwa Na Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Ikiwa Halmashauri Hiyo Inachukua Asilimia Ya Fedha Inayotoka Kwenye Kodi Ya Sumatra Elfu 22 Ambayo Madereva Wote Wanaridhia Kuilipa Kwa Hiari Yao.
Wakitoa Ufafanuzi Kwa Madereva Wenzao Viongozi Wa Bodaboda Wilaya Ya Njombe Akiwemo Katibu Wao Fred Ndelwa Na Julius Chatanda Wamewaomba Madereva Hao Kutulia Na Kulipa Kodi Ya Sumatra Wakati Swala La Kodi Ya Maegesho Likijadiliwa Mezani Na Viongozi Wa Sumatra Na Halmashauri Jambo Ambalo Limepingwa Vikali Na Madereva Hao.
Akizungumza Kaimu Afisa Sumatra Mkoa Wa Njombe Denis Maghembe Amesema Kuwa Kodi Ya Sumatra Ipo Kisheria Na Hivyo Wamiliki Wa Vyombo Vya Moto Wanatakiwa Kulipia Kwa Mujibu Wa Sheria Huku Akisema Swala La Kodi Nyingine Inayolalamikiwa Ya Maegesho Atakwenda Kufanya Mazungumzo Na Watalaamu Wa Halmashauri Kuona Namna Ya Kuiondoa .
Bwana Maghembe Amesema Zoezi La Operation Ya Kukamata Pikipiki Ambazo Hazijalipia Kodi Ya Sumatra Limesimamishwa Kwa Muda Hadi Wafikie Mwafaka Baada Ya Majadiliano Na Viongozi Wa Pande Zote Zinazohusika Na Ukusanyaji Wa Kodi Na Vyombo Vya Ulinzi Na Usalama Ili Kuona Wanavyoweza Kupunguza Baadhi Ya Kodi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment