Monday, February 27, 2017
HOSPITALI YA ILEMBULA KUTOA HUDUMA ZA MATIBABU YA MACHO
NJOMBE
Hospitali Inayomilikiwa Na Kanisa La Kiinjili La Kiluthel Tanzania Ilembula Imeanza Zoezi La Kutoa Elimu Kwa Wananchi Wa Mkoa Wa Njombe Kwaajili Ya Kuwapeleka Wagonjwa Wa Macho Ili Wakapimwe Na Kutibiwa Tatizo La Macho Linalowakabili Zaidi Wazee.
Akizungumza Daktari Wa Macho Ambaye Ni Mratibu Wa Macho Katika Hospitali Ya Ilembula Dkt Erick Msigomba Amesema Kuwa Hospitali Hiyo Imeweka Madaktari Bingwa Wa Matatizo Ya Macho Ambao Wanafanya Upasuaji Wa Jicho Na Kuweka Lensi Nyingine Kwa Kutumia Mashine Za Kisasa.
Dkt Msigomba Amesema Kuwa Uongozi Wa Hospitali Hiyo Umeamua Kuanza Zoezi La Kutoa Elimu Kwa Wananchi Na Viongozi Mbalimbali Kwa Kushilikiana Na Watalaamu Wa Halmashauri Za Mkoa Wa Njombe Ambapo Wameanza Kutembelea Zahanati,Vituo Vya Afya Na Hospitali Ili Kuwabaini Wenye Matatizo Hayo Na Kuwapatia Huduma Za Matibabu.
Dkt Msigomba Amesema Kuwa Halmashauri Zinatakiwa Kuonesha Ushirikiano Wa Kueleimisha Wagonjwa Wa Macho Kwamba Huduma Zinapatikana Katika Hospitali Ya Ilembula Ambapo Hata Kwa Wenye Bima Za Afya Nayo Wanapata Huduma Hizo Kwa Mujibu Wa Miongozo Ya Wizara Ya Afya Inavyosema.
Akizungumza Kwa Upande Wake Mwenyekiti Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Valentino Hongori Amesema Kuwa Taarifa Hiyo Ni Muhimu Kwa Madiwani Wote Kuipokea Na Kuifanyia Kazi Kwa Kushiriki Kuhimiza Wananchi Wenye Matatizo Ya Macho Kufika Katika Hospitali Hiyo Ili Wakapatiwe Huduma Ya Matibabu Kuliko Kukaa Na Matatizo Hayo Nyumbani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment