MENEJA UPLANDS FM ELMATHEW KIKA AKISUBIRI KUOKOLEWA BAADA YA KUNASA KWENYE MIBA WAKATI AKIFANYA USAFI
JITIHADA ZA KUMUOKOA AKIWA AMENASA KWENYE MIBA ZIKIENDELEA RICHARD ELLY MSIGWA ANAMSAIDIA KUMUOKOA.
WARIDI MASEKO AKIWA NA WAFANYAKAZI WENGINE WA RADIO UPLANDS FM
WAFANYAKAZI WA UPLANDS FM WAKIWA NA BAADHI YA WANANCHI WA MTAA WA NAZARETH WAKIFANYA USAFI SIKU YA JUMAMOSI YA KWANZA YA MWEZI
MTENDAJI WA MTAA WA NAZARETH ESIYO MPETE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUFANYA USAFI
NJOMBE
Wafanyakazi wa Uplands Fm radio wameungana na wananchi mjini Njombe kufanya zoezi la usafi wa mazingira ili kuunga mkono agizo la serikali la kufanya usafi huo kila juma mosi ya mwisho ya mwezi.
Wakizungumza wakati wa kufanya usafi huo katika barabara ya Kuelekea Nazareth Cetre baadhi ya wananchi na wananchi wa mtaa wa Nazareth wamesema kila mwananchi anatakiwa kutambua umuhimu wa zoezi hilo na kufanya kwa kujituma wenyewe bila kusukumwa.
Wamesema usafi ni jukumu la kila mmoja kutekeleza kwenye maeneo yao kila siku ili kuepuka mlipuko wa magonjwa yanayoweza kusababishwa na uchafu wa mazingira huku wakisema changamoto kubwa na kukosekana kwa kutupa taka na kulazimika kuziteketeza kwa moto.
Akizungumza na Uplands Fm wakati zoezi la usafi likiendelea afisa mtendaji wa mtaa wa Nazareth Esiyo Mpete amesema mwamko wa wananchi na taasisi umekuwa mkubwa licha ya kuwa baadhi bado hawajawa na moyo wa kujitoa kushiriki zoezi hilo.
Bwana Mpete amesema ushiriki huo unatakiwa kuendelezwa hata kwa mwaka huu wa 2017 huku viongozi mbalimbali nao wakitakiwa kuendelea kuwahimiza wananchi kufanya usafi kwenye maeneo yao ambapo kamati za afya zinatarajia kupita nyumba kwa nyumba kukagua usafi wa mazingira.
No comments:
Post a Comment