AFISA MFAWIDHI WA SUMATRA MKOA WA NJOMBE AYUBU JUMA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI OFISINI KWAKE
NJOMBE
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Nchi kavu Na majini Nchini Sumatra Mkoa wa Njombe imepiga marufuku tabia za baadhi ya madereva wanaosafarisha abiria kuanzia saa tisa usiku kinyume na utaratibu uliowekwa na serikali.
Afisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoa wa Njombe Ayubu Juma amesema magari yote ya abiria yanatakiwa kuanza safari zake kuanzia saa kumi na mbili alfajiri ili kuondoa usumbufu wa abiria kutembea usiku ambapo hatua kali zitakuchukiliwa kwa madereva watakaokwenda kinyume.
Katika Hatua Nyingine Afisa Sumatra Juma amesema wamiliki na makampuni ya magari ya usafirishaji abiria Mkoa wa Njombe wanatakiwa kufanya usafiriji abiria katika barabara za Lupembe, Ludewa,Igwachanya ambako magari yaliyopo ni ya kampuni moja.
Amesema kuwepo kwa makampuni tofauti ya usafirishaji abiria kwenye barabara moja kunasaidia kupunguza malalamiko ya abiria ambao wamekuwa wakilalamikia kusumbuliwa na makondakta na kutothaminiwa kwa kupewa kauli mbaya na wasafirishaji hao.
Kwa magari yatakayokiuka utaratibu wa Sumatra wa kuondoka wakati wa usiku nje ya saa kumi na mbili iliyopangwa na mamlaka hiyo abiria wanatakiwa kupiga simu kwa afisa sumatra kupitia namba 0767591959 hata kwa matatizo mbalimbali yanayohusu changamoto za usafiri.
Baadhi ya Abilia wa Kata za Mavanga Wilaya ya Ludewa na Barabara ya kuelekea Lupembe Wilaya ya Njombe na Wanging'ombe Wamelalamikia kitendo cha magari kutoka Usiku huku wakienda mbali zaidi kwamba magari ya kuelekea barabara ya Lupembe yanachelewa kuondoka katika kituo cha Kibena.
No comments:
Post a Comment