Mkuu
wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizungumza katika mkutano wa Wadau wa
Afya uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Meru,kushoto ni Mganga
Mkuu wa mkoa,Dk frida Mokiti.
Nteghenjwa Hosseah, Arusha
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dokta Frida Mokiti amesema kuwa uhaba wa vituo
vya afya katika maeneo ya pembezoni mwa miji umekua ukichangia vifo vya
mama wajawazito na watoto kutokana na kutembea umbali mrefu kutafuta
huduma hiyo.
Akizungumza
katika Kikao kazi cha Mkoa kinachojadili hali ya afya ya mkoa, Dr.
Mokiti amesema kuwa juhudi za makusudi zinahitajika kuhakikisha kuwa
huduma za afya kwa mama na mtoto zinapatikana kwa urahisi ili kupunguza
tatizo hilo ambalo limekua likirudisha nyuma afya ya wakina mama pamoja
na kukatisha maisha yao.
Akizungumza
katika Kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amewaagiza
Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuhakikisha kuwa wanajenga Kituo cha Afya
katika kila tarafa ili kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi pia
amewataka viongozi kuweka mipaka katika maeneo ya zahanati ili kuepuka
uvamizi wa maeneo hayo yanayowahudumia watu.
“Wakati
sasa umefika wa kuhakikisha tunatokomeza kabisa changamoto hii ya vifo
vya mama na mtoto, inasikitisha sana kuona mama anafariki wakati wa
kujifungua kwa sababu tu amekosa huduma ya afya karibu na makazi
yake,lazima tuwalinde na kuwajali wananwake, kwa sababu bila ya wao
kujifungua hata sisi tusingekuwepo” Alisema Gambo.
Aliongeza
kuwa Kila Halmashauri ihakikishe inatenga Fedha kwenye mapato yake ya
ndani halkadhalika Ruzuku toka Serikali Kuu ielekezwe kwenye Miradi ya
Afya na tuendelee kutafuta wadau watakaotusaidia katika utekelezaji wa
miradi hii bila kusahau uhamasishaji wa nguvu za wananchi kwa Pamoja
tutatokomeza tatizo hili.
Kwa upande wake Mkazi wa Arusha Hussein Igunge na Mkuu wa Wilaya ya
Longido Mhe. Daniel Chongolo wameitaka serikali iboreshe huduma za
afya ikiwemo upatikanaji wa madawa kwa wale waliokata bima ili waweze
kunufaika na bima zao pamoja na uhaba wa watumishi katika sekta ya afya.
Mganga
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Dk Frida Mokiti akizungumza katika mkutano wa
Wadau wa Afya uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Meru,kulia ni
Mkuu wa mkoa,Mrisho Gambo akimsikiliza kwa makini,kushoto ni Katibu
Tawala wa wilaya ya Karatu na Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Richard
Kwitega.
Baadhi ya Watalaam wa sekta ya afya wakiwa kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Meru mkoa wa Arusha.
Baadhi
ya viongozi wa dini walioshiriki mkutano huo wakisikiliza kwa makini
pia waliahidi kushirikiana na mfuko wa Bima ya Afya(NHIF)kuhamasisha
waumini wao kujiunga na mfuko wa CHF.
Wakuu
wa wilaya za mkoa wa Arusha wakiwa kwenye mkutano huo uliojadili kwa
kina mikakati ya kuinua sekta ya Afya kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya
ya Arusha,Gabriel Daqarro,Mkuu wa wilaya ya Monduli,Idd Kimanta na Mkuu
wa wilaya ya Karatu,Theresia Mahongo.
No comments:
Post a Comment