Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, October 13, 2016

WANANCHI WA MUNGATE WAMGOMEA DIWANI WA KATA YA MDANDU NA MHANDISI WA WILAYA KUPELEKA MAJI KIJIJI CHA ITAMBO:WAWATOA MPUTAMPUTA WASIANDIKE MIHTSARI BAADA YA KIKAO KUMALIZIKA OFISINI HAPO




 
 WANANCHI WA KIJIJI CHA MUNGATE WAKIWA KWENYE KIKAO CHA NDANI KUJADILI SWALA LA KUTOA MAJI KWENYE TENKI LA MAJI YA TOVE MTWANGO KWENYE KITONGOJI CHA CHALUHANGA KIJIJI CHA ITAMBO KWA MADAI WAO WENYEWE WANAUHITAJI WA VITUO 16 KWENYE VITONGOJI VYA KIJIJI CHA MUNGATE DIWANI WATAKA KUPELEKA KIJIJI KINGINE WAGOMA YASITOKE MAJI KWENYE TENKI LAO VINGINEVYO WATAFUTE VYANZO VINGINE VYA MAJI.

 
 MHANDIS WA MAJI WILAYA YA WANGING'OMBE SALM ISSA AKIFAFANUA JUU YA UTAFITI WAO WALIOTUMWA KWAMBA WATAFITI KAMA MAJI YATATOSHA KUPELEKA KWENYE KIJIJI HICHO WANANCHI WASEMA HIZO SIASA WAKIRUHUSU MAJI KUPELEKWA HUKO WATAKUJA PATA MATATIZO YA KUKOSEKANA KWA MAJI KIJIJI HAPO SIKU ZA USONI



 MWENYEKITI WA KIJIJI CHA MUNGATE ALFRED MLELWA AKIAHIRISHA KIKAO CHA JUMUIYA YA MAJI MUNGATE BAADA YA KUGOMEA DIWANI ASIPELEKE MAJI KIJIJI CHA ITAMBO NA KUTISHIA KUWAKAMATA WATAKAOONEKANA WANACHIMBA MITARO YOYOTE NDANI YA KIJIJI CHAO HICHO.







 MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WATUMIA MAJI YA TOVE MTWANGO WA VIJIJI 15 CHONGORO SANGA AKITOLEA UFAFANUZI WA KIKAO KILICHOPITA KWAMBA NACHO HAKIKUKUBALIANA KUPELEKA MAJI KATIKA KIJIJI HICHO YA KUTOKA TOVE MTWANGO
 DIWANI WA KATA YA MDANDU ANNAUPENDO GOMBELA BAADA YA WANANCHI HAO KUMTUHUMU KWAMBA AMEANDAA SHEREHE NA WANANCHI WA ITAMBO KWAMBA MAJI YATAPELEKWA KWA KUWA WANANCHI WA MUNGATE WAMEKUBALI KUTOA MAJI HAYO NA HAPA ANAKANUSHA KWAMBA TAARIFA HIZO SI ZA KWELI NI ZA UONGO HAKUNA SHEREHE YOYOTE ILIYOANDALIWA ITAMBO.

 HAPA WANANCHI NA WAJUMBE WA JUMUIYA YA WATUMIA MAJI MUNGATE WAKIWATOA MKIKIMKIKI VIONGOZI WALIOKUWEMO NDANI YA KIKAO HICHO AKIWEMO DIWANI  ANNAUPENDO GOMBELA NA MHANDIS WA MAJI KWAMBA OFISI YA KWAO HAWARUHUSIWI KUENDELEA KUBAKI NDANI HUMO

 DIWANI HUYO ANNAUPENDO  GOMBELA AKIZUNGUMZA NA BAADHI YA WANANCHI WACHACHE JUU YA HALI ALIYOIONA KIJIJINI HAPO MUNGATE


NJOMBE

Wananchi wa  Kijiji cha Mngate Wilayani Wanging’ombe wamegomea mradi wa maji Tove usipelekwe kitongoji cha Chaluhanga kijiji cha Itambo kwa madai katiba yao hairuhusu kuongeza kijiji kingine nje ya vile 15.

Wakizungumza kwenye kikao cha Jumuiya ya Watumia maji wa kijiji cha Mungate wamesema hawawezi kuruhusu Uongozi wa halmashauri na kata kuchukua maji ya tenki la kijiji hicho na kupeleka kijiji cha Itambo ikiwa kijiji chao hakijakidhi matakwa ya maji.

Wananchi hao wamesema migogoro mingi ambayo imekuwa ikitokea inasababishwa na viongozi kuchanganya siasa na maendeleo na kutaka mhandis wa maji Wilaya ya Wanging’ombe kutafuta chanzo kingine cha kuchukua maji yaende kwenye kijiji cha Itambo.

Diwani wa kata ya Mdandu Anna Upendo Gombela amesema kijiji cha Itambo kilikuwepo kwenye ratiba ya kufikishiwa maji  na wafadhili waliotekeleza mradi wa maji Tove kwani hadi sasa kuna mabomba yapo hayajatumika jambo ambalo limepingwa vikali na wananchi wa Mungate.

Muhandis wa maji Wilaya ya Wanging’ombe Salmu Issa  amesema maji yamradi wa Tove yaliopo  kijiji cha Mungate yanatoshereza kupeleka kwenye kijiji cha Itambo kitongoji cha Chaluhanga na kwamba hakuna sababu ya kutafuta chanzo kingine ikiwa kwenye tenki la Tove Mtwango yapo.

Mwenyekiti wa jumuiya ya watumia maji ya Tove Mtwango Chongoro Sanga amesema mwenye mamlaka ya kuruhusu maji kwenda katika kitongoji cha Cha Chaluhanga Kijiji cha Itambo  ni wananchi wa kijiji Cha Mungate ambao wanalinda miundominu ya maji na wanaojua idadi ya watumia maji waliopo na siyo vinginevyo.

No comments:

Post a Comment