Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, October 17, 2016

MKUU WA WILAYA LUDEWA AWATAKA WATALAAMU WA MAJI NA WANANCHI KULINDA VYANZO VYA MAJI



LUDEWA

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa  Andrea Tsere amewataka wataalamu wa halmashauri kushirikiana na viongozi wa kata na vijiji kutunza vyanzo vya maji na kuacha kuchungia mifugo na kulima kwenye vyanzo hizo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu huyo wa Wilaya bwana Tsere wakati akizungumza na Uplands Fm kuhusiana na tatizo la kukosekana kwa maji katika maeneo ya shule,zahanati na kusema amekwisha waagiza wataalamu wa maji kutumia sheria ndogondogo zilizopo ili kutunza vyanzo vya maji.

Bwana Tsere ameagiza  viongozi  wanaosimamia vyanzo vya maji kutoa kipaumbele kupeleka maji kwenye shule na zahanati na kusema kuwa itakapobainika kuna kiongozi hawajibiki ipasavyo katika kutunza vyanzo vya maji ataanza kuwachukulia hatua kali za kisheria viongozi wenyewe.


Akizungumza kwa upande wake Diwani wa kata ya Mlangali Hamis Kayombo amesema katika kata hiyo wamehimiza utunzaji wa vyanzo vya maji ambao umeanza kutekelezeka kwa baadhi ya maeneo ambapo kata hiyo inakabiliwa na tatizo la kukosekana kwa maji na jitihada za kusogeza maji hayo zimeanza.

Awali wakizungumza  wananchi wa kata ya Mlangali Wilaya ya Ludewa wameiomba halmashauri kuwasaidia kupeleka fedha kwaajili ya kuwaunga mkono katika mradi wa maji wanaoutekeleza kwenye kijiji cha Litundu utakaohudumia karibu kata nzima ya  Mlangali huku wakiunga mkoano utunzaji wa vyanzo vyake.

No comments:

Post a Comment