DIWANI WA KATA YA RAMADHANI GEOGE MENSON SANGA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSIANA NA TUKIO LA KIKATILI LA KUPIGWA MWANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MBOGAMO MJINI NJOMBE AMBAYE AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA KIBENA HADI SASA.
HUYU NI DIWANI WA KATA YA MJIMWEMA AMBAYE PIA NI MWENYEKITI WA CHADEMA WILAYA YA NJOMBE ABUU MTAMIKE AKIZUNGUMZA BAADA YA KUSHUHUDIA MWANAFUNZI HUYO AKIWA WODINI AKIENDELEA NA MATIBABU
NJOMBE
Mkuu wa wilaya ya Njombe Luth Msafiri amelaani vikali tukio la kupigwa na kuumizwa vibaya mikono na sehemu nyingine za mwili kwa mwanafunzi Eliza Sifukwe anayesoma kidato cha nne katika shule ya sekondari Mbogamo iliyopo kata ya Ramadhani.
Kauli hiyo Ya Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Msafiri imetolewa kufuatia walimu sita wa shule hiyo ambao wanashikiliwa na jeshi la polisi akiwemo Mkuu wa shule ya sekondari Mbogamo Helmina Mgaya kumshambulia mwanafunzi wa kidato cha nne Elizabeth Simfukwe mkazi wa mbozi mkoani Songwe kwa kosa la kukutwa na simu kinyume na sheria za shule hiyo.
Bi. Msafiri amesema walimu sita wa shule ya sekondari Mbogamo akiwemo Mkuu wa shule hiyo Bi.Helmina Mgaya wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumpatia adhabu kupita kiasi na kumsababisha madhara ya mwili wa mwanafunzi Elizabeth Simfukwe ambaye amelazwa katika hospitali ya kibena.
Akizungumza akiwa ofisini kwake Mganga mfawidhi wa hospitali ya kibena Dkt Cerina Nyoni Amethibitisha kumpokea mwanafunzi wa shule ya sekondari Mbogamo Eliza Simfukwe ambaye alipigwa na walimu sita mnamo tarehe sita mwezi Octoba mwaka huu baada ya kukutwa na simu ya mkononi ikiwa kwenye sanduku lake bwenini.
Mtandao huu umemutafuta Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Njombe kwa njia ya simu Bi.Pudenciana Plotas ambaye amekili kuwashikilia walimu hao na kusema kwa sasa wanaendelea na uchunguzi dhidi ya tukio hilo la kupigwa kwa mwanafunzi huyo.
Kwa Upande Wake mkurugenzi wa shule ya Sekondari Mbogamo bwana Tonya Mgaya alipopigiwa simu kutolea ufafanuzi juu ya tukio la mwanafunzi huyo amesema hawezi kuzungumzia chochote kwa kuwa tukio hilo lipo mikononi mwa jeshi la polisi.
Diwani wa kata ya Ramadhani Geoge Sanga ametaka wanafunzi waliopo shuleni kwa sasa wanatakiwa kuendelea na masomo kwaajili ya kujiandaa na mtihani wa Taifa wakati mwanafunzi mwenzao akiendelea na matibabu Hospitali ya Kibena huku Diwani wa Kata ya Mjimwema Abuu Mtamike akiomba hatua kali zichukuliwe Dhidi ya walimu hao.
Kwa upande wake Kaimu afisa elimu Shule za sekondari wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Anton Mtweve akiwa katika hospitali hiyo amesema hana taarifa zozote za kulazwa kwa mwanafunzi huyo na kwamba Hospitalini hapo alikwenda kwaajili ya kumuangalia Ndugu yake ambaye amelazwa na siyo kwaajili ya mwanafunzi huyo ambapo kumekuwa na usiri Mkubwa kwa viongozi wa serikali kutoa taarifa za tukio la kupigwa kwa walimu hao.
No comments:
Post a Comment