MKUU WA WILAYA YA LUDEWA ANDREA T'SELE
MKUU WA WILAYA YA LUDEWA ANDREA TSERE AKISALIMIANA NA MADIWANI WALIOKUWEPO KWENYE KIKAO HICHO
MWENYEKITI WA SACCOS MLANGALI WA MUDA NATHANAEL MGANI AKITOLEA UFAFANUZI KWA BAADHI YA VIPENGELE VYA KWENYE KATIBA YA CHAMA HICHO
DIWANI KATA YA MLANGALI AKIZUNGUMZA MBELE YA MKUU WA WILAYA KWENYE KIKAO CHA WANACHAMA WA SACCOS YA MLANGALI
MKUU HUYO WA LUDEWA TSERE AKIAGIZA KUCHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA WALIOHUSIKA NA ULAJI FEDHA ZA CHAMA CHA AKIBA NA MIKOPO
HUYU NI MWENYEKITI WA BODI YA SACCOS YA MLANGALI WILLY HAULE AKIWA KWENYE KIKAO HICHO
KULIA NI MENEJA WA SACCOS YA MLANGALI OSWARD MSAFIRI NA KUSHOTO NI MWENYEKITI WA SACCOS WILLY HAULE WAKITUHUMIWA KUHUSIKA NA UPOTEVU WA FEDHA ZA SACCOS HIYO PAMOJA NA WENZAO AMBAO HAWAPO HAPA
LUDEWA
Mwenyekiti wa bodi ya saccos mlangali na meneja wake
wanashikiliwa na jeshi la polisi Wilaya
ya Ludewa kwa tuhuma za kutumia
vibaya fedha na mali za chama cha
ushirika cha akiba na mikopo cha mlangali .
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere ameagiza
watuhumiwa Willy Haule ambaye ni mwenyekiti wa bodi na Osward Msafiri meneja wa
saccos ya mlangali kushikiliwa kuanzia jana hadi hapo uchunguzi utakapo
kamilika wakiwa gerezani kwa tuhuma za upotevu wa mali za chama ikiwemo misitu
ya miti.
Kufuatia kushikiliwa na jeshi la polisi kwa
watuhumiwa hao Bwana Tsere amelikabidhi jeshi la polisi saccos ya mlangali
kuilinda na kuchunguza mali zote za chama wakishilikiana na viongozi wa muda wa
bodi ya saccos hiyo wakati watuhumiwa wakiwa rumande hadi tarehe ndani ya mwezi
mmoja na wakibaini ubadhilifu umefanywa na viongozi hao watafikishwa
mahakamani
kujibu tuhuma zinazowakabili.
Aidha Tsere ametumia fursa hiyo kuliagiza jeshi la polisi
kuwasaka wanachama wasiyofika kwenye mkutano wa chama na ambao wanadaiwa na
saccos ikiwa hawajarejesha deni wanalodaiwa ili warejeshe fedha hizo ndani ya
siku 30 huku akiagiza kumtafuta popote alipo mhasibu wa chama hicho aunganishwe
na viongozi wenzake.
Wakijitetea mbele ya mkutano mkuu watuhumiwa wa sakata hilo
Willy Haule mwenyekiti wa bodi na Osward Msafiri Meneja wa saccos ya Mlangali
wamekana kuhusika na tuhuma za ubadhilifu wa fedha hizo kwa madai zilipotea
wakati akiwa meneja marehemu Ludrof Chaula maarufu kacheche ambaye alikuwa
diwani aliyefariki kwa kujinyonga mwaka 2012 baada ya kugudua dosari ya
shilingi milioni 42 za chama hicho.
Wanachama wakiwa kwenye mkutano mkuu waemesema pesa
nyingine zilizopotea ni za ufuatiliaji wa madeni ya wanachama waliokopa ambao
walikuwa bado hawajarejesha deni lao huku riba ikiwa mara mbili ya mkopo wake.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya Andrea Tsere
ameivunja
bodi na watumishi wa chama cha ushirika cha akiba na mikopo cha mlangali
kutokana na viongozi wake kutuhumiwa kutumia vibaya fedha za chama hicho.
Bwana Tsere ametoa Uamuzi huo wa kuivunja bodi na
kufukuza watumishi wa saccos hiyo baada ya kusikiliza malalamiko ya wanachama
zaidi ya tisini wakiwatuhumu viongozi
wao kuhusika na ubadhilifu wa fedha zaidi ya shilingi milioni mia moja.
Aidha Tsere amewatoa hofu wanachama wa saccos ya mlangali kwamba hakuna
mwanachama yeyote atakayedhulumika haki zake zilizopo kwenye chama hicho na kuitaka bodi ya muda iliyoundwa kusimamia
saccos hiyo isifutwe kuhakikisha baada ya tarehe 30 mwezi novemba inaanza kazi
ya kuendesha shughuli zake kama kawaida.
Awali Mwenyekiti wa muda wa bodi ya saccos ya
mlangali Nathanael Mgani amesema wanachama wa saccos hiyo wamewiwa
kumshilikisha mkuu wa wilaya hiyo katika kutafuta ufumbuzi wa migogoro
inayowakabili baada ya kuona fedha walizoweka kwenye chama chao zimeliwa na
watu wachache.
Baadhi ya wanachama wa saccos mlangali wamelalamikia viongozi wao kwa kudhuruma fedha za chama pamoja na
kuwakata fedha za amana,fedha za hisa za wanachama kinyume na utaratibu.
No comments:
Post a Comment