MBUNGE WA JIMBO LA LUPEMBE JORAM HONGORI ALIPOKUWA AMETEMBELEA MPAKA WA NJOMBE NA MOROGORO NA KUAMBIWA MPAKA WAKE NI MTO MFUJI NA SIYO KAMA INAVYOELEZWA KWA SASA NA WENGINE.
HUU NI MTO MFUJI AMBAO UNADAIWA KUWA NI MPAKA WA MKOA WA MOROGORO NA NJOMBE
NJOMBE
Mbunge wa jimbo la Lupembe ameahidi kutatua mgogoro wa mipaka baina ya wananchi wa madeke Mkoani Njombe na mkoa wa Morogoro kwa kumuita Waziri wa ardhi ,nyumba na makazi ili amalize tofauti zilizopo.
Kuli hiyo ya Mbunge wa lupembe Joram Hongori ameitoa wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Madeke kwenye mkutano wa hadhara uliolenga kuwajulisha mipango ya serikali katika kutekeleza miradi iliyopo.
Mwalimu Hongori amesema anakwenda kumuita waziri wa Ardhi,nyumba na makazi William Lukuvu ili afike Kwenye jimbo la Lupembe kumaliza tofauti zilizopo za wananchi waliopo mpakani mwa Mkoa wa Njombe na Morongoro .
Awali wakiuliza maswali mbalimbali kwa Mbunge huyo wananchi wa kijiji cha madeke wametaka kufahamu serikali imejiandaaje kutatua mgogoro wa mipaka kati ya Morogoro na Njombe kwa vijiji vya Madeke na nyamate ambavyo vinadaiwa mpaka wake ni mto Mfuji huku Wakihoji maswali mbalimbali yakiwemo ya miundombinu ya barabara.
Mbunge Hongori amefika kwenye mto Mfuji ambao umedaiwa kuwa ndiyo mpaka wa mikoa hiyo miwili na kutaka wananchi waliopo kwenye mpaka huo kuvumilia wakati jitihada za kumleta waziri huyo zikiendelea ili kupata ufumbuzi wa mgogoro huo.
No comments:
Post a Comment