GARI LIKIWA KWENYE VUMBI LA BARABARANI
HII NI BARABARA AMBAYO WANANCHI WAMELALAMIKIA KWAMBA HAIJAMWAGIWA MAJI WALA KUSHINDILIWA NA KUSABABISHA VUMBI KUONGEZEKA
vumbi la kwenye barabara hiyo
Wananchi wa kijiji cha Havanga kata ya kidegembye wilayani Njombe wameiomba halmashauri hiyo kurudia kutengeneza barabara ya Havanga Idunda kwa kushindilia na kumwagia maji kuliko ilivyo kwa sasa.
Rai hiyo imetolewa na wananchi wa kijiji hicho kufuatia kukithili kwa vumbi ambapo wametoa kilio chao kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge wa jimbo la Lupembe Joram Hongori alipotembelea katika kijiji hicho kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa.
Wamesema halmashauri ya Wilaya ya Njombe Kupitia Mhandis wake wa ujenzi wamelima barabara hiyo bila kuwagia maji na kushindilia na kusababisha madhara kwa wananchi hususani pindi magari yakipita yanatimu vumbi kama unavyotazama kwenye picha hizo.
Akijibu mwaswali ya wananchi hao Mbunge wa jimbo la Lupembe Joram Hongori ameahidi kufuatilia kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Njombe Ili kuhakikisha wanarudia kuitengeneza barabara hiyo kwa kushindilia na kumwagia maji barabara hiyo kwa kiwango kinachostahili.
Hongori amesema serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni nane kwaajili ya kutengeneza barabara ya Kibena hadi madeke kwa kiwango cha lami ili kuondoa adha inayowakuta wananchi wa lupembe kwa kipindi hicho na msimu wa kusafirisha mazao na pia barabara hiyo itaunganisha na Mkoa wa Morogoro -Mlimba.
No comments:
Post a Comment