KATIBU WA CHAMA CHA WALIMU MKOA WA NJOMBE FRATERN KWAHHISON AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE LEO
WANAFUNZI WAPO KWENYE MCHEZO WANAOELEKEZWA NA MWALIMU WAO BAADA YA KUTOKA DARASANI
MWALIMU MWALONGO WA SHULE YA MSINGI MPECHI AKIZUNGUMZA KUHUSIANA NA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI
MWALIMU AKIWACHEZESHA WANAFUNZI KWA KUNYOSHA VIUNGO BAADA YA KUTOKA DARASANI
NJOMBE
Serikali Mkoani Njombe inakabiliwa na deni la zaidi
ya shilingi milioni 900 za malimbikizo mbalimbali ya mishahara ya walimu ya mwaka 2015 na 2016 ikiwemo fedha za uhamisho pindi
wanapohamishiwa sehemu nyingine.
Kauli hiyo imetolewa na katibu wa chama cha
walimu mkoa wa Njombe Mwalimu Fratern Kwahhison
wakati akizungumza na mtandao huu kuhusiana na siku ya mwalimu Duniani
ambayo Kitaifa Chama hicho huadhimisha baada ya miaka mine.
Mwalimu Kwahhison amesema sherehe hiyo inatoa fursa
kwa walimu kuwasilisha madai na changamoto mbalimbali kwa serikali ili kuishinikiza iweze kuwatatulia
kwa wakati na walimu hao wafanye kazi katika mazingira yasiyo na manung’uniko
yoyote.
Amesema walimu wa Tanzania wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo kulipwa mshahara mdogo
usiyokidhi mahitaji
yao,kutopandishwa madaraja na kurekebishiwa mishahara,kutolipwa madeni yao na
kushindwa kuwajengea nyumba za kuishi ambapo walimu wengi wanatoka umbali mrefu
wa kilomita zaidi ya tano.
Mwalimu Kwahhison amebainisha viwango tofauti
vinavyodaiwa na walimu kwenye halmashauri za Mkoa wa Njombe kuwa serikali inadaiwa na walimu wa mji wa
Makambako milioni 30580900,Wilaya ya Njombe inadaiwa milioni 38386800, Wilaya
ya makete inadaiwa shilingi milioni 223946516,Halmashauri ya wilaya ya ludewa
inadaiwa shilingi milioni 419089346,Wanging’ombe milioni 188603507,na
Halmashauri ya Mji wa Njombe inadaiwa shilingi milioni 254645090 madai hayo
yote ni sehemu tu kwani bado wanaendelea kukusanya madai hayo.
Mwalimu huyo Kwahhison amesema madai hayo ni yale ya
Likizo,ya matibabu,upandishwaji madaraja,uhamisho,kuwasafirisha walimu wastaafu
baada ya kumaliza kipindi chao cha utumishi serikalini,madai ya shughuli
maalumu pindi wanapoitwa na mwajili wao, kujikimu,ajira mpya,mazishi na mapunjo nakwmaba jumla ya shilingi milioni mia tisa ishilini na tisa na sabini na tano elfu mia sita na hamsini na tisa {929075659} ambayo ni sehemu ya madai walio yakusanya.
Kwa upande wao baadhi ya walimu mjini Njombe wametaka serikali kuwaboreshea
mazingira ya kufanyia kazi ikiwemo vitendea kazi ,kuongeza idadi ya walimu kwa
baadhi ya shule zenye walimu wachache
pamoja na kuwajengea nyumba za kuishi ili kufundisha vizuri wanafunzi.
Mashirika ya UNESCO na ILO Yalianzisha siku ya mwalimu Duniani mwaka 1994 lengo likiwa ni siku ya kumbukumbu na kutafakari
madhila wanazopata walimu katika
utumisho wao kutokana na waajili wakorofi
ambao hawataki kuwapa haki.
Maadhimisho hayo kwa mwaka huu hapa nchini yamefanyika kwa
baadhi ya mikoa ukiwemo mkoa wa Luvuma yakiwa na Kauli mbiu inayosema Mwalimu athaminiwe .
Imeandaliwa na Michael Ngilangwa- Njombe
No comments:
Post a Comment