Kufuatia
kitendo cha askari namba F. 3016 SGT Talib Hamad Kassim ambaye tayari
amefukuzwa kazi na Jeshi la Polisi kwa kitendo chake cha kuomba na
kupokea rushwa kutoka kwa raia wa kigeni mjini Zanzibar, Jeshi la
Polisi nchini linalaani vikali tabia hiyo na kwamba ni tabia ya askari
binafsi na siyo maadili ya askari wa Jeshi la Polisi.
Kutokana na kitendo hicho, tayari
Jeshi la Polisi limemfukuza kazi askari huyo na atafikishwa mahakamani
kwa hatua zaidi za kisheria. Aidha, Jeshi la Polisi litaendelea kuchukua
hatua kali dhidi ya askari wake yeyote atakayekiuka maadili yake ya
kazi.
Jeshi la Polisi nchini
halitamuonea muhali askari yeyote atakayekwenda kinyume na maadili ya
kazi na kutenda vitendo binafsi vinavyo lifedhehesha au kulitia dosari
Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
No comments:
Post a Comment