NJOMBE
Wachezaji wa mpira wa migu 20 wa kutoka kijiji cha
Nyombo kata ya Ikuna Wilayani Njombe
hapo jana wamenusurika kupoteza uhai baada ya gari walilokuwa wamepanda kuacha
njia na kuanguka katika eneo la zahanati ya kijiji cha Ikuna.
Wakizungumza na Uplands fm wachezaji hao ambao kwa
sasa ni majeruhi wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Kibena kwaajili ya
matibabu wamesema walikuwa wakitokea kijiji cha Nyombo kuelekea maduma kwaajili
ya kuchezo wa kirafiki na timu ya maduma.
Wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari
walilokuwa wamepanda aina ya canter
ambapo baada ya ajali hiyo dereva wake alitokomea kusiko julikana
kutokana na ajali hiyo iliyosababisha wengine kukatwa vidole vya mikononi na
wengine kuumia vibaya sehemu mbalimbali za miili yao.
Akizungumza na Uplands fm Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
Kibena Cerina Nyoni Amethibitisha
kupokea majeruhi 20 waliopata ajali
kutoka kijiji cha Ikuna na kwamba hali zao zinaendelea vizuri baada ya kupatiwa
huduma za matibabu hospitalini hapo.
No comments:
Post a Comment