NJOMBE
Mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Nazareth Elias Mdendemi amefariki dunia asubuhi ya leo huku majeruhi mmoja Tino Makweta wote wakazi wa mjimwema akipelekwa hospitali ya kibena kwaajili ya matibabu baada ya kugongwa na gari lenye namba za usajili T 726 CJM .
Wakizungumza wakiwa eneo la tukio baadhi ya Mashuhuda wamesema gari hilo lilikuwa likitokea barabara ya Songea Njombe ambapo majira ya saa moja asubuhi tukio hilo liliweza kutokea na kusababisha mmoja kufariki na mwingine kujeruhiwa walipokuwa wakitaka kuvuka barabara hiyo.
Kwa upande wao mashuhuda wa ajali hiyo wameomba serikali kuwawekea matuta na kutaka maafisa usalaama wa barabarani kuwepo eneo hilo ili kuimarisha usalama wa watembea kwa miguu wanaoelekea Nazareth .
Akizungumza na uplands fm mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mjimwema Andrea Mligo amewaomba watumiaji wa vyombo vya moto kuwajali watembea kwa miguu hususani watoto huku wazazi na walezi nao wakitakiwa kuwasindikiza hadi shuleni watoto wao ili kuwapatia usalama zaidi wakiwa barabarani.
Kaimu mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Njombe Dkt Allen Oden Kitalu amethibitisha kupokea majeruhi mmoja na mwili mmoja wa mwanafunzi aliyegongwa eneo la Nazareth na kupoteza uhai wake na kusema kuwa majeruhi bado anaendelea na matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment