KAIMU MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA ABRAHAMU KAAYA AKIWA NA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE LUTH MSAFIRI ALIPOWATEMBELEA WANUFAIKA WA TASAF
HAWA NI WANUFAIKA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI KATA YA KICHIWA NA ,MTWANGO
HAPA MKUU WA WILAYA AKIWA KIJIJI CHA ITUNDUMA KATA YA MTWANGO
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE LUTH MSAFIRI AKIZUNGUMZA NA WANUFAIKA WA TASAF KIJIJI CHA ITUNDUMA
MKUU WA WILAYA ANASALIMIANA NA WAZEE KICHIWA
MKUU HUYO WA WILAYA ANAGAWAI MAANDAZI NA BAGIA KWA WATOTO AMBAO WAZAZI WAO WALIFIKA KUCHUKUA VYETI VYA KUZALIWA ZAHANATI YA ITUNDUMA
MRATIBU WA TASAF WILAYA YA NJOMBE CASSIAN NKUNGA AKIMKARIBISHA MKURUGENZI ILI AMKARIBISHE MKUU WA WILAYA KUZUNGUMZA NA WANUFAIKA WA KIJIJI CHA KICHIWA
NJOMBE
Wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini Tasaf Wilayani
Njombe wametakiwa kuanzisha miradi ya ufugaji, na kilimo kupitia pesa
wanazopewa ili mpango huo utakapokwisha wawe na maendeleo kiuchumi.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Luth
Msafiri wakati akiongea na wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini Tasaf
wa vijiji vya kata ya Kichiwa ambapo amesema mpango huo ni wa miaka mitatu
hivyo wanufaka watumiye fursa hiyo kuibua miradi hiyo.
Bi. Msafiri amesema
kutokana na wanufaika kupewa pesa hizo watendaji wa vijiji na watalaamu
wa mifugo wanatakiwa kuwatembelea wanufaika hao ili kusaidia kutoa ushauri na
kutibu mifugo iliyoanzishwa kupitia fedha hizo kwaajili ya kuepusha hasara za
kufa kwa mifugo huku akitaka fedha hizo zisitumike kununulia pombe .
Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya Mratibu wa
tasaf wa halmashauri ya Wilaya ya Njombe
Cassian Nkunga amesema fedha
zinazotolewa na tasaf zimeanza kuonesha matunda kwa baadhi ya wanufaika kwani
wengine wameanzisha ufugaji kuku huku na Nguruwe.
Kwa upande wao wanufaika wa fedha za tasaf
Wakizungumza mbele ya mkuu wa wilaya huyo wameshukuru kwa hatua ya serikali kuwakumbuka na kutoa shuhuda mbalimbali kwamba
wengine wamenunua kuku na nguruwe,wengine wakitumia kuwanunulia sare za shule
watoto na shughuli za kilimo na
matibabu.
No comments:
Post a Comment