KATIBU TAWALA MKOA JACKSON SAITABAHU AKITOA HOTUBA YAKE YA UZINDUZI WA UTAFITI WA MAAMBUKIZI MAPYA YA VIRUSI VYA UKIMWI KWA MKOA WA NJOMBE KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI
MENEJA WA TAKWIMU MKOA WA NJOMABE BWANA Israel Mwakapalalal akitoa maelezo mafupi juu ya zoezi la Utafiti ambalo linakwenda kuanza siku chache za usoni.
WADAU WALIOSHIRIKI UZINDUZI HUO HII LEO WAKIWEMO MAKATIBU TAWALA WA WILAYA ZA MKOA WA NJOMBE AMBAO UZINDUZI HUO UMEFANYIKA
Kiongozi wa kitengo cha mawasiliano ICAP Bi.Mihayo Bupamba Akiwasilisha mada kwa wadau juu ya Utafiti huo ambao unatarajia kuleta manufaa makubwa ya takwimu za maambukizi kwa wakazi wa Njombe na Watanzania kwa Ujumla
KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMABE JACKSON SAITABAHU AKIZUNGUMZA WAKATI WA UZINDUZI WA MPANGO WA UTAFITI WA MAAMBUKIZI MAPYA YA VIRUSI VYA UKIMWI KWA MKOA WA NJOMBE LEO KATIKA UKUMBI WA WAUGUZI KIBENA
NJOMBE
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi amewataka viongozi na vyombo vya habari mkoani Hapa kufikisha ujumbe sahihi kwa kaya zilizochaguliwa kwaajili ya kupima afya zao huku wananchi nao wakitakiwa kujenga mazoezi ya kupima afya zao katika maeneo yao.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu tawala Mkoa Jackson Saitabahu Kwa Niaba ya Mkuu wa mkoa wa Njombe wakati wa Uzinduzi wa zoezi la utafiti wa maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi kwa wadau wa afya wakiwemo viongozi wa dini na watalaamu wa afya ambapo wanatakiwa kuzielimisha kaya hizo ili kuisaidia serikali kupata takwimu sahihi za maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Saitabahu amesema Nafasi ya Viongozi wa Dini na vyombo vya habari ni muhimu kwa lengo la kuelimisha kaya zilizoteuliwa kwaajili ya utafiti huo nakuwasihi wananchi wote kujitokeza kupima afya katika maeneo yao ili kujua afya kwani kuchelewa kupata matibabu ni kuhatarisha afya zao.
Kwa upande wake Kiongozi wa kitengo cha mawasiliano ICAP Bi.Mihayo Bupamba amesema zoezi la utafiti wa takwimu za maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI Litafanyika kwa kipindi cha miezi nane kwa nchi nzima ambapo Njombe ina maeneo 18 ya utafiti ikiwemo Halmashauri ya Mji na wilaya Njombe, Makete,Makambako,Ludewa na Wilaya ya Wanging'ombe.
Akizungumza kwa niaba ya ofisi ya taifa ya Takwimu meneja takwimu Mkoa wa Njombe Israel Mwakapalalal amesema uzinduzi wa zoezi la utafiti linafanyika kila mkoa hapa Nchini na kusema upimaji huo wa kwenye utafiti utaambatana na kupima magonjwa mengine ikiwemo kaswende na matatizo ya Ini.
Katika utafiti huo Unaofanywa na serikali kupitia Wizara ya Afya,maendeleo ya jamii,jinsia na watoto kaya Elfu 16 zitafanyiwa utafiti wa maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI na maeneo 525 kwa Nchi nzima ambapo utafiti huo wa kwenye kaya zilizochaguliwa zitapimwa afya zao kwa hiari.
No comments:
Post a Comment