Wednesday, October 26, 2016
MKURUGENZI CHUO KIKUU HURIA ATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA ZA ELIMU KUJIANDAA NA MACHIMBO YA MIGODI YA LIGANGA NA MCHUCHUMA
MKURUGENZI WA CHUO KIKUU HURIA TANZANIA TAWI LA NJOMBE DKT SUSAN GWALEMA AKITOA TAARIFA YA CHUO HICHO KITUO CHA NJOMBE
NJOMBE
Serikali Mkoani Njombe Imetakiwa kushirikiana na wadau kuwaandaa vijana katika nyanja mbalimbali kuhusiana na shughuli zitakazoanza kufanyika kwenye machimbo ya migodi ya liganga na mchuchuma kwa kuanzia na matumizi ya lugha na shughuli za ujasiliamali.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa chuo kikuu huria Tawi la Njombe Dkt Suzana Gwalema wakati akizungumza kuhusiana na vijana kujiunga na chuo hicho ili kuongeza taaluma na ujuzi kwaajili ya maandalizi ya fursa zitakazokuwepo mara zoezi la machimbo ya migodi hiyo litakapoanza.
Dkt Gwalema amesema chuo kikuu huria tawi la Njombe kinaandaa mtaala wa ujasiliamali kwaajili ya kufundishia vijana waliohitimu elimu ya sekondari ya kidato cha nne ambao utahusisha kozi ya tehama na kozi ya Utalii itakayokuwa na lugha za kigeni ikiwemo ya kichina.
Katibu tawala msaidizi sehemu ya uzarishaji na Uchumi Mkoa wa Njombe Lameck Noa amesema serikali inaendelea kuhamasisha wananchi kujiandaa na machimbo ya migodi ya liganga na mchuchuma kwaajili ya kupata fursa za masoko kutokana na ugenzi utakaokuwepo ambao utahitaji vyakula na mahitaji mengine muhimu .
Baadhi ya Wadau wa maendeleo Akiwemo padre wa kanisa katholiki jimbo la njombe meledius mlowe amesema maandalizi ya msingi ya mgodi yanatakiwa kufanyika kikamilifu kwa kuwalipa fidia wananchi wa eneo husika la machimbo huku vijana wakitakiwa kujipanga na uzarishaji mkubwa katika miradi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment