NJOMBE
Wananchi mkoani Njombe wametakiwa kujiunga kwenye vikundi vya ujasilia mali kwa lengo la kuzitazama fursa mbalimbali za maendeleo ya uchumi kwa kulima kilimo biashara na kuanzisha miradi ya ufugaji ili kubadilisha maisha yao kiuchumi.
Akizungumza mkurugenzi wa Kampuni ya wakala wa ushauri katika kilimo biashara Ya Namaingo Bi.Ubwa Ibrahimu amesema kampuni hiyo imekuwa ikitoa ushauri kwa wakulima kuacha kilimo cha mazoea na kulima kilimo biashara kitakacho wainua kiuchumi.
Bi.Ibrahimu amesema kampuni ya Namaingo imekuwa ikiwaelimisha wananchi juu ya kurasimisha biashara zao na ardhi walio nayo,kutoa elimu ya mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na kutoa elimu ya biashara na kujitambua kuangalia fursa zilizopo kwa kuanzisha ufugaji kuku,nyuki,sungura,samaki na mbogamboga.
Amesema Kampuni ya Namaingo inatarajia kuanzisha miradi ya ufugaji nyuki kibiashara katika mikoa ya Njombe na Mbeya kwa vikundi vilivyo chini ya kampuni hiyo ambapo miradi hiyo inafanywa kikanda na wataitafutia soko na viwanda ili kuunga mkono juhudi za Rais Magufuri za kuanzisha viwanda.
Bonifasi Ngole ni mkazi wa Magoda Mjini Njombe amesema kampuni ya Namaingo imewanufaisha wajasilia mali kwa kuwapatia elimu mbalimbali za Ufugaji na kilimo biashara ambacho kinawasaidia kuinua uchumi na kufahamu fursa za kupatikana kwa masoko pamoja na kurasimisha biashara zao ziweze kufahamika.
No comments:
Post a Comment