Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, October 25, 2016

MADIWANI WILAYA YA NJOMBE WAAGIZA KUCHUKULIWA HATUA WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI WALIOANISHA MGOMO BARIDI WA KUKUSANYA MAPATO







MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE VALENTINO HONGOLI AKIZUNGUMZA NA MADIWANI KWENYE KIKAO CHA  BARAZA LA MADIWANI LEO
NJOMBE

Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Njombe Wamemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya Watendaji wa Vijiji Na Kata ambao wameanzisha mgomo baridi wa kutokusanya mapato ya mizigo katika maeneo yao.

Akizungumza mbele ya madiwani hao mwenyekiti wa kamati ya Huduma na Uchumi Julius Salingwa amesema mapato yameshuka kutokana na watendaji kuanzisha mgomo baridi wa kutosimamia ukusanyaji wa mapato huku akitaka mwenyekiti na mkurugenzi kuchukua hatua kwa watendaji wenye mgomo huo.

Salingwa amesema watendaji wengine wamegoma kukusanya mapato kutokana na kukosa maslahi ambapo ameomba Mkurugenzi kuwaita watendaji hao ili kufanya mazungumzo nao juu ya ukusanyaji huku akitaka kuimarisha ulinzi maeneo yanayovujisha mapato yakiwemo ya Ikuna, Mtwango na maeneo mengine.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Ya Njombe Valentino Hongoli ameomba watendaji wa kata kupeleka taarifa za watendaji walioanzisha mgomo wa kutokusanya mapato hayo na kusema halmashauri nayo imebaini tatizo hilo baada ya kuona mbao zinazotozwa ni chache kuliko zilizopakiliwa.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bi.Monica Kwiluhya ameahidi kuimarisha usimamizi mkali wa mapato kuanzia kesho kwa kutembelea maeneo Ya mapato usiku na mchana na kutaka watendaji kufanya kazi ya serikali ipasavyo vinginevyo  hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.


Awali watendaji wa kata wakizungumzia tuhuma hiyo ya Mgomo baridi iliyoelezwa na madiwani wamesema changamoto kubwa wafanyabiashara wanapitisha mazao na mbao wakati wa usiku na wakati mwingine changamoto ya usafiri inasababisha kushindwa kufuatilia mapato kikamilifu.

No comments:

Post a Comment